Nenda kwa yaliyomo

Wenseslaus I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Wenseslaus katika kanisa kuu la Mt. Vitus, Prague.
Kardinali Miloslav Vlk akitembeza fuvu la kichwa la Mt. Wenseslaus katika maandamano ya tarehe 28 Septemba 2006.
Sanamu ya Mt. Wenseslaus katikati ya mji wa Prague.

Wenseslaus I (kwa Kicheki Václav, ˈvaːtslaf[1]; 907 hivi - 28 Septemba 935) alikuwa mtawala (kníže)[2] wa Bohemia tangu mwaka 921 hadi alipouawa na watu waliotumwa na mdogo wake, Boleslaus I.

Alilelewa katika hekima ya kiutu na ya Kimungu na bibi yake Ludmila. Ingawa alikuwa mkali kwake mwenyewe, alikuwa mpenda amani katika kuendesha nchi na mwenye huruma kwa fukara. Alikomboa watumwa wengi Wapagani waliokuwa wanauzwa huko Praha, ili wafikie ubatizo. Kisha kukabili matatizo mengi katika kuongoza na kuinjilisha wananchi wake, aliuawa kanisani[3].

Anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.[4][5][6]

Kikanisa cha Mt. Wenseslaus katika kanisa kuu la Mt. Vitus.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Septemba[7][8][9]. Nchini Ucheki ndiyo sikukuu ya taifa.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Christiansen, Rupert. "The story behind the carol: Good King Wenceslas", The Telegraph, 14 December 2007
  2. Mershman,Francis. "St. Wenceslaus." The Catholic Encyclopedia Vol. 15. New York: Robert Appleton Company, 1912. 8 January 2016
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/29350
  4. Describing the Codex Gigas, a thirteenth-century manuscript from Bohemia in the Swedish National Library in Stockholm, it is stated: "All this bears witness to the outstanding importance of the cult of Vaclav in Bohemia at the time of the Devil's Bible's compilation. Moreover, all three festivals are inscribed in red ink, denoting their superlative degree."
  5. Within a few decades of Wenceslas' death four biographies of him were in circulation.The First Slavonic Life (in Old Church Slavonic), the anonymous Crescente fide, the Passio by Gumpold, bishop of Mantua (d. 985), and The Life and Passion of Saint Václav and his Grandmother Saint Ludmilla by Kristian.
  6. Hastening Toward Prague: Power and Society in the Medieval Czech Lands - Lisa Wolverton - Google Boeken. Books.google.com. 2001-07-25. Iliwekwa mnamo 2013-11-20.
  7. Martyrologium Romanum
  8. September 28/October 11 Archived 29 Novemba 2014 at the Wayback Machine.. Orthodox Calendar (PRAVOSLAVIE.RU).
  9. Martyr Wenceslaus the Prince of the Czechs. OCA - Lives of the Saints.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.