Nenda kwa yaliyomo

Tembo wa vita

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka War elephant)
Tembo wa vita (picha ya Kihindi)
Tembo wakivuta mizinga - Uhindi mwaka 1906

Tembo wa vita (kwa Kiingereza: war elephant) ni tembo anayetumiwa kwa mapigano ya vita.

Hapo walifundishwa kwanza kubeba watu, kufuata amri na kuzoea kelele na msongamano wa watu.

Kazi ya tembo vitani ilikuwa hasa kutisha maadui, kuvunja mistari ya wanajeshi na kuvuruga utaratibu wao kwenye mapigano[1].

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Matumizi ya tembo wa vita yalianza huko Bara Hindi mnamo mwaka 2000 KK[2], lakini yalienea hadi kwingine.

Mfalme Pyrrhus wa Epirus (Ugiriki)[3] aliwatumia sana, vilevile Hannibal wa Karthago. Hannibal alifaulu kuvuka milima ya Alpi pamoja na tembo na kushambulia Jamhuri ya Roma[4].

Katika Ulaya ya Kale na Asia ya Magharibi, mikakati ya kijeshi ilisahihishwa haraka jinsi ya kudhibiti tembo wa kivita kwa kushambulia wanyama hao kwa moto au kuwajeruhi mapema. Hata hivyo, katika Uhindi na Asia ya Kusini majeshi yaliendelea kutumia tembo hadi karne ya 19 ambapo matumizi ya mzinga yalifanya tembo kuwa bila faida.

Baadaye tembo waliendelea kutumiwa kwa shughuli za kubeba mizigo ya kijeshi.

Aina ya tembo

[hariri | hariri chanzo]

Wanyama waliotumiwa kwa makusudi hayo walikuwa hasa tembo wa Asia (spishi elephas) na pia tembo wa Afrika kaskazini ambao hawako tena. Tembo wa Afrika wa kisasa (spishi loxodonta) walitumiwa tu mara chache; kuna ushuhuda katika historia ya milki ya Axum [5].

Tembo wa vita kwenye mapigano, picha ya mawe kwenye kaburi la Buddha huko Sanchi, Uttar Pradesh.[6]

Mapokeo ya Kiislamu

[hariri | hariri chanzo]

Katika historia ya Uislamu kuna habari za tukio linalokumbukwa kama Am al-Fil yaani "mwaka wa tembo" lilIlotokea mnamo 570 BK. Mwaka ule mfalme Mkristo Abraha kutoka Yemen alivamia sehemu nyingine za Uarabuni akalenga Makka. Aliingia na jeshi kubwa pamoja na tembo wa vita ama mmoja au wanane. Tembo aliyeitwa Mahmud alisimama kwenye mipaka ya Makka akakataa kuendelea. Inasemekana katika mwaka ule mtume Muhammad alizaliwa.

  1. Kigezo:Cite dictionary Also: elephantry (Wiktionary)
  2. "History Of The Domestication Of Animal". Historyworld.net. Iliwekwa mnamo 2018-05-21.
  3. Encyclopædia Britannica ("Pyrrhus") 2013.
  4. Prevas, John (1 Machi 2009). Hannibal Crosses the Alps: The Invasion of Italy and the Punic Wars. Perseus Books Group. ISBN 978-0-7867-3121-3.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link), p. 86
  5. The Elephants of Aksum: In Search of the Bush Elephant in Late Antiquity
  6. Asiatic Mythology by J. Hackin pp. 83ff

Kujisomea

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]