Walter von Saint Paul-Illaire
Walter von Saint Paul-Illaire au Adalbert Emil Walter Le Tanneux von Saint Paul-Illaire (Berlin, Januari 12, 1860 - Berlin, Desemba 12, 1940) alikuwa ofisa wa wilaya ya koloni la Ujerumani katika Afrika Mashariki (Afrika Mashariki ya Kijerumani).
Familia yake, Le Tanneux von Saint Paul, ilikuwa ya kisharifu kutoka zamani sana, na ilihamia Prussia katika karne ya 17. [1]
Maua ya aina ya 'viola' au 'violet' (kwa Kiajemi: بنفسج) katika jenasi Saintpaulia, yalipewa jina lake baada ya kuonekana katika matembezi yake ya Milima ya Usambara mwaka wa 1893. Alituma mbegu ya maua hayo kwa Hermann Wendland, mtaalamu wa botania wa Ujerumani, na Mkuu wa bustani ya Kifalme, bustani za Herrenhausen huko Hannover. Huyo alitoa habari ya kwanza ya mimea hiyo, na aliita mimea hii Usambara veilchen ('Violeti ya Usambara'). [2] [3]
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Baba wa Walter von Saint Paul-Illaire, Ulrich von Saint Paul-Illaire (1833-1902), alikuwa ofisa katika jeshi la wanamaji na mwanachama wa Dola la Ujerumani (kwa Kijerumani: Deutsches Reich). Baba yake alipendezwa sana na miti, hasa miti ya misunobari, na alimwuliza kwa barua na George Engelmann, daktari na mwanabotania wa Missouri, maelezo ya anzisho na uwezo wa kutumia miti kati ya misunobari inayoitwa Engelmann spruce. Labda upendo wake wa botania ulimtia mtoto wake, Walter, hamu ya kun'gamua mimea.[4] [5] .
Mnamo 1885, Walter von Saint Paul-Illaire alikuwa mshiriki wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki(Kijerumani: Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft(DOAG)). Januari 1886, yeye alsafiri nchini Kenya ya leo.[6] Baadaye, mwaka wa 1889, alikua mkurugenzi wa forodha na wakala mkuu wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki huko Zanzibar(Unguja). Mnamo 1891, Dola la Ujerumani (Kijerumani: Deutsches Reich) lilishika usimamizi wa Afrika Mashariki ya Ujerumani. St. Paul-Illaire alianza kufanya kazi ya ofisa ya wilaya ya Tanga kutoka 1891 mpaka 1900.[7] Wakati huu alipenda kutembea katika milima na miamba ya Usambara, karibu na Tanga, na alifurahi sana kuona mimea hii, pamoja na rangi ya samawati ya maua yake. Jina la spishi, ionantha, limetokana na Kigiriki, 'ίον', kwa ajili ya rangi ya zambarau, na 'άνθος', ambayo inamaanisha maua.[8]Siku hizi mmea huu umejumuishwa ndani ya jenasi ya Streptocarpus.[9]
Katika jukumu lake la ukoloni, alishughulika katika masuala ya kazi katika koloni ya Afrika Mashariki ya Ujerumani,[10] na pia alitoa hoja kuondoa na kuwatenga Wahindi wa koloni kwa sababu walikuwa idadi kubwa ya watu wa rangi waliofanya biashara ya rejareja na Waafrika, na kwa wengi, alibishi walitumia vitabu vya hesabu bila kufuata kawaida ya Ulaya.[11] Saint Paul-Illaire alikuwa pia mwandishi wa kikoloni wa gazeti la Cologne, Kölnische Zeitung, na mwaka wa 1896 alichapisha kamusi ya Kiswahili. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, katika hotuba chini ya jina la "Africanus", aliomba wajumbe wa Amerika na wa Britania kwenye Mkutano wakuleta Amani(1919-1920), huko Paris, warudishe makoloni ya Ujerumani.[12] [13]
Kifo
[hariri | hariri chanzo]Alifariki huko Berlin mnamo 1940, akazikwa katika makaburi ya Invalidenfriedhof kulekule, lakini kaburi lake halijahifadhiwa. [14] "Aligundua" mimea ya maua ya 'violeti ya Kiafrika' yeye, lakini ilikuwa mashuhuru duniani, kama mimea ya vyungu, baada ya kifo chake.
Machapisho
[hariri | hariri chanzo]- Swahili-Sprachführer. Daresalaam 1896. [15]
- Kriegs-Xenien: Stimmen und Stimmungen aus dem Weltkriege. Leipzig 1919.
- Der Fluch der deutschen „Gewissenhaftigkeit“. Berlin 1921.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Genealogisches Handbuch des Adels, Adelslexikon Band XIV, Band 131 der Gesamtreihe, C. A. Starke Verlag, Limburg (Lahn) 2003, ISSN 0435-2408, S- 319–320
- ↑ Eastwood, A., et al. “THE CONSERVATION STATUS OF SAINTPAULIA.” Curtis's Botanical Magazine, vol. 15, no. 1, 1998, pp. 49–62. JSTOR, www.jstor.org/stable/45065280. Accessed 4 June 2021.
- ↑ "Early Discovery and Naming | Gesneriad Reference Web".
- ↑ "Correspondence Saint Paul-Illaire (Ulrich) and Engelmann (George)" https://ia600500.us.archive.org/16/items/mobot31753004062557/mobot31753004062557.pdf
- ↑ "Picea engelmannii (Engelmann spruce) description".
- ↑ Wie Deutsch-Ostafrika entstand : mit dem Bildnis des Verfassers und einer Karte / von Dr. Carl Peters Liepzig 1912. http://lbsopac.rz.uni-frankfurt.de/CMD?ACT=SRCHA&IKT=6015&DB=30&TRM=ppn:402491491
- ↑ Ulrich van der Heyden: Koloniales Gedenken im Blumentopf: Das Usambara-Veilchen und sein „Entdecker“ aus Berlin, in: Ulrich van der Heyden und Joachim Zeller (Hrsg.): Kolonialismus hierzulande – Eine Spurensuche in Deutschland. Sutton Verlag, Erfurt 2007, ISBN 978-3-86680-269-8, S. 220–222.
- ↑ "Origins of African Violets and Impatiens". pss.uvm.edu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-02-11. Iliwekwa mnamo 2021-07-27.
- ↑ "The Great Merger – Current Taxonomic Status | Gesneriad Reference Web".
- ↑ Die Arbeiterfrage in Deutsch-Ostafrika; W. von St. Paul Illaire: Deutsche Kolonialzeitung › 26 (1909) › 4 (23.1.1909) p57 - 59 https://sammlungen.ub.uni-frankfurt.de/kolonialbibliothek/periodical/pageview/7864168?query=illaire
- ↑ Zur Indierfrage in Deutsch-Ostafrika; WaIter v. St. Paul-Illaire: Jahrbuch Uber die deutschen Kolonien, Jahrg. 3 (1910) p. 254-263 https://brema.suub.uni-bremen.de/dsdk/periodical/titleinfo/1996560
- ↑ "The adjustment of the German colonial claims; dedicated to the American and British delegates of the Peace conference" https://archive.org/details/adjustmentofgerm00afririch/page/n1/mode/2up
- ↑ Deutsche Bücherei (Leipzig): Weltkriegssammlung Erscheinungsdatum: 1918 http://d-nb.info/576354082
- ↑ "Walter of Saint Paul-Illaire - ZXC.wiki".
- ↑ "Kolonialbibliothek / Swahili-Sprachführer".