Wakartusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Badge of the Carthusian Order
Monasteri ya zamani huko Seville, Hispania.
Ramani ya nyumba ya Kikartusi ya kawaida (Clermont), iliyochorwa na Eugène Viollet-le-Duc mwaka 1856.
Jinsi Francisco de Zurbarán alivyomchora askofu Hugo wa Grenoble akitembelea Kartusi.

Shirika la Wakartusi, au Shirika la Mt. Bruno, ni utawa mmojawapo wa Kanisa Katoliki. Wamonaki wake wote, wanaume kwa wanawake wanaishi ndani kwa ndani: wengine katika nyumba za binafsi, wengine katika makao ya pamoja.

Shirika lilianzishwa na Bruno Mkartusi mwaka 1084.

Linafuata sheria zake, badala ya kanuni ya Benedikto wa Nursia inayoongoza wamonaki karibu wote wa Kanisa la Kilatini.

Jina linatokana na milima ya Chartreuse (nchini Ufaransa), ambapo Bruno na wakaapweke wenzake 6 walijenga makao ya kwanza.

Kaulimbiu ya shirika ni: Stat crux dum volvitur orbis (kwa Kilatini "Msalaba unadumu wakati ulimwengu unabadilikabadilika."

Hatua upwekeni[hariri | hariri chanzo]

Nyumba za Wakartusi leo[hariri | hariri chanzo]

Leo duniani ziko nyumba 25 za Wakartusi; kati yake 5 ni za masista. Kwa jumla wako wamonaki 370 wanaume na 75 wanawake. Monasteri hizo ziko Argentina (1), Brazil (1), France (6), Germany (1), Italy (4), Ureno (1), Slovenia (1), South Korea (2), Spain (5), Uswisi (1), Ufalme wa Muungano (1) na Marekani (1).[1]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. To view complete list and images of the Monasteries visit: "The charterhouses in the world". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-10-20. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2010.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: