Nenda kwa yaliyomo

Vitenzi vishirikishi vikamilifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mifano
  • Sada alikuwa mtoro shuleni
  • Mahmoud ni mchokozi
  • Mahmoud si mchokozi
  • Mariam ana gari zuri
  • Ndoo imo kisimani

Vitenzi vishirikishi vikamilifu (alama yake ya kiisimu ni: t) ni maneno ambayo yamekamilika, yaani, hayaambatanishwi na mofimu/ kiambishi / silabi / neno au kitenzi kingine. Vitenzi hivi pia hugawanyika katika makundi madogomadogo.

Uchambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Kuna mizizi sita ya vitenzi vishirikishi vikamilifu.

(i) -KUWA

[hariri | hariri chanzo]

Endapo utakuwa na kitenzi cha mzizi wa -kuwa kimesimama/kimekaa peke yake katika sentensi na kimetoa taarifa kamili - basi hicho ni kitenzi kishirikishi.

Mifano
  • Sada alikuwa mtoro shuleni
  • Wanjiru atakuwa mgeni rasmi
  • Nguruka amekuwa mshindi wetu
  • Anna alikuwa mwimbaji hodari
  • Mohamed hakuwa mlevi
  • Sisi tutakuwa wanafunzi bora

Hiki ni kitenzi kishirikishi kinachojulisha uyakinishi wa tendo. Kitenzi hiki hujulisha kuwepo kwa uhusiano baina ya vipashio vya lugha.

Mifano
  • Mahmoud ni mchokozi
  • Tembo ni mnyama mkali
  • Wanjau ni mwanafunzi mtiifu
  • Anna ni mwimbaji hodari

(iii) SI

[hariri | hariri chanzo]

Hiki ni kitenzi kishirikishi kinachojulisha ukanushi wa tendo. Kitenzi hiki hujulisha kuwepo kwa uhusiano baina ya vipashio vya lugha.

Mifano
  • Mahmoud si mchokozi
  • Tembo si mnyama mkali
  • Wanjau si mwanafunzi mtiifu
  • Anna si mwimbaji hodari

(iv) Vitenzi vishirikishi vinavyojulisha umiliki

[hariri | hariri chanzo]

Hivi ni vitenzi vinavyotoa taarifa ya umiliki kwa nomino au kiwakilishi.

Mifano
  • Mariam ana gari zuri
  • Chakula kina chumvi nyingi
  • Ulimi hauna mfupa
  • Husna ana mme mzuri
  • Darasa letu lina vumbi
  • Chatu hana meno

(v) Vitenzi vishirikishi vya viambishi vya mahali (po, mo, ko)

[hariri | hariri chanzo]

Hivi ni vitenzi vinavyotoa taarifa ya mazingira ya tendo husika. Mazingira hayo ni pamoja na kuwa nje, ndani, juu ya, au katika eneo fulani.

Mifano
  • Ndoo imo kisimani
  • Kikombe kiko mezani
  • Wanafunzi wamo darasani
  • Yeye yumo chumbani
  • Fedha zimo kabatani
  • Jembe lipo shambani

(vi) Kitenzi kishirikishi chaa viambishi vya ngeli vikisimama peke yake

[hariri | hariri chanzo]

Hivi ni vitenzi vinavyobainisha maana ya ngeli ikisimama peke yake.

Mifano
  • Ndoo i kisimani
  • Kikombe ki mezani
  • Wanafunzi wa darasani (hapa ni lazima sauti ibadilike ili kutoa maana tofauti na ile maana ya kiwakilishi/kivumishi cha -a unganifu). Bimaana ya kwamba wakati unataja wanafunzi wa - kwenye wa lazima ufanye kama unasimama vile...
  • Yeye yu chumbani
  • Fedha zi kabatani
  • Jembe li shambani

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vitenzi vishirikishi vikamilifu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.