Visiwa vya Shetland
Shetland (au Visiwa vya Shetland) ni funguvisiwa upande wa kaskazini ya Uskoti (Scotland). Inahesabiwa kuwa sehemu ya Uskoti.
Visiwa vya Shetland viko baharini kati ya Visiwa vya Faroe na Visiwa vya Orkney. Visiwa vikubwa zaidi huitwa Mainland, Yell, Unst, Fetlar, Whalsay na Bressay.
Kwa jumla kuna visiwa 100 na kati yake 16 vinakaliwa na watu 22,920[1]. Wengi wana asili ya Uskoti. Karibu nusu ni Wakristo, hasa Waprotestanti. Wengine wengi hawana dini yoyote.
Makao makuu ya utawala na mji mkubwa ni Lerwick. Mji wa pili unaitwa Scalloway nao ni kitovu cha kihistoria.
Eneo
[hariri | hariri chanzo]Funguvisiwa hili liko mpakani kati ya Bahari Atlantiki upande wa magharibi na Bahari ya Kaskazini upande wa mashariki.
Eneo la nchi kavu ni km² 1,426 na theluthi mbili zake ni eneo la kisiwa cha Mainland.
Tabianchi ni nusu aktiki na si baridi sana kutokana na athira ya mkondo wa ghuba.
Mwinuko wa juu ni kilima cha Ronas Hill chenye kimo cha mita 449 juu ya usawa wa bahari.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Uchumi wa visiwa unategemea uvuvi, kilimo na hasa ufugaji wa kondoo.
Mwaka 1969 mafuta ya petroli yaligunduliwa yakawa chanzo kipya cha mapato.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Makadirio ya mwaka 2019.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Shetland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |