Nenda kwa yaliyomo

Fetlar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Shetland
Mahali pa Shetland kati ya Uskoti na Norwei

Fetlar ni kisiwa cha funguvisiwa ya Shetland, upande wa kaskazini ya Uskoti (Scotland). Inahesabiwa kuwa sehemu ya Uskoti.

Visiwa vya Shetland viko baharini kati ya Visiwa vya Faroe na Visiwa vya Orkney. Funguvisiwa hii iko mpakani kati ya Bahari Atlantiki upande wa magharibi na Bahari ya Kaskazini upande wa mashariki.

Tabianchi ni nusu aktiki na si baridi sana kutokana na athira ya mkondo wa ghuba.

Uchumi wa visiwa unategemea kilimo na hasa ufugaji wa kondoo.

Mwaka 1969 mafuta ya petroli yaligunduliwa yakawa chanzo kipya cha mapato.