Nenda kwa yaliyomo

Vielezi vya namna

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Vielezi vya namna au jinsi)
Mifano
  • Mary anaimba vizuri
  • Wafanyabiashara wanauza jumla
  • Ndondi si mchezo mzuri sana
  • Kidawa anatembea harakaharaka
  • Joshua anakula polepole

Vielezi vya namna (alama yake ya kiisimu ni: E) ni maneno yanayotoa taarifa au ufafanuzi ambao unaenelezea namna au jinsi kitenzi (tendo) kinavyofanyika. Maneno haya hujulisha kuwa kitenzi hicho kinatumika namna gani au jinsi gani.

Uchambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Vielezi hivi vya namna au jinsi pia vimegawanyika katika makundi madogomadogo sita

Mifano ya jumla

[hariri | hariri chanzo]
  • Mtoto huyu analia sana
  • Mariamu anaimba vizuri
  • Kiiza anatembea polepole
  • Johnson amelala kifudifudi
  • Mwajuma anaongea kitoto

(I) Vielezi halisi

[hariri | hariri chanzo]

Hivi ni vielezi vya namna au jinsi ambavyo huwa kwa dhati yake hutoa taarifa ihusuyo kitenzi.

Mifano
  • Nyoka anakimbia sana
  • Khadija anaandika vizuri
  • Wafanyabiashara wanauza rejareja
  • Angel amejikwatua mno
  • Aliendelea kusoma zaidi ya rafiki yake

(II) Vielezi vinavyofafanua vivumishi

[hariri | hariri chanzo]
Mifano
  • Watoto wamemuua nyoka mkubwa sana (watoto = nomino, wamemuua = kitenzi kikuu, nyoka = nomino, mkubwa = kivumishi cha sifa, sana = kielezi).
  • Chris amenunua nyumba nzuri sana
  • Subira amepika chakula kitamu sana
  • Ndondi si mchezo mzuri kabisa

(III) Vielezi vya KI- ya mfanano

[hariri | hariri chanzo]
Mifano
  • Aidan anatembea kitoto (Aidan = nomino, anatembea = kitenzi kikuu, kitoto = kielezi cha ki- ya mfanano, yaani ile kitoto!)
  • Shehoza aliadhabiwa kikoloni
  • Okelo anaongea kiungwana
  • David amevaa kihuni

(IV) Vielezi vya hali

[hariri | hariri chanzo]

Hivi ni vielezi vya namna au jinsi ambavyo vina uhusiano na tabia ya kitu. Nomino za dhahania zinapotumika kufafanua kitenzi huwa kielezi.

Mifano
  • Ndege huruka upesi angani (Ndege = nomino, huruka = kitenzi kikuu, upesi = nomino dhahania ilivyobalishwa kuwa kielezi)
  • Barabara zetu zimejengwa upya
  • Gari hili hukimbia kwa kasi

(V) Vielezi viigizi

[hariri | hariri chanzo]

Hivi ni vielezi vya namna au jinsi ambavyo hufuatisha/huiga mlio unatokea baada ya tendo kutendeka.

Mifano
  • Risasi imepenya fyuuu! (risasi = nomino, imepenya = kitenzi kikuu, fyuu! = kielezi kiigizi cha tukio husika).
  • Loveness amebweteka bwee!
  • Maji yamemwagika mwaa!
  • Mti umekatika tii!/puu!

(VI) Vielezi vikariri/vibariki/viradidi

[hariri | hariri chanzo]
Mifano
  • Michael amelala kifudifudi (Michael = nomino, amelala = kitenzi kikuu, kifudifudi = kielezi cha namna au jinsi katika mzizi wa vikariri au vibariki)
  • Husna anaandika kibatabata
  • Godfrey anatembea harakaharaka
  • Mwinyimvua anakula polepole
  • Jirani anatembea kinyumenyume

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vielezi vya namna kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.