Ugonjwa wa Parkinson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ugonjwa wa Parkinson (kwa Kiingereza: Parkinson's_disease) ni ugonjwa wa ubongo ambapo mtu hukosa homoni ya dopamini. Hili hufanyika baada ya seli zinazotengeneza dopamini kuharibika.

Dalili ya ugonjwa huu ni kutetemeka kwa mikono (hand tremors), pamoja na shida ya kutembea. Huenda pia mtu akawa na shida za kufikiria. Wagonjwa wa Parkinson huwa na huzuni, utovu wa usingizi pamoja na wasiwasi mwingi.

Ugonjwa huu ulipewa hili jina baada ya anayeaminika kuwa mvumbuzi James Parkinson aliyeandika mengi kuhusu wagonjwa wenye ugonjwa huu katika maandishi aliyoyaita 'An Essay on the Shaking Palsy'.

Kiini cha ugonjwa wa Parkinson[hariri | hariri chanzo]

Haijulikani haswa kiini cha ugonjwa huu kutokea lakini yakisiwa kwamba hurithiwa kutoka kwa kizazi hadi kingine. Sababu za kimazingira huweza pia kuchangia ugonjwa huu; kwa mfano yasemekana kwamba wanaofanya kazi za kupuliza kemikali kwa mimea huenda wakaupata kwa urahisi. Wanaume huwa kwa hatari kubwa kuupata ugonjwa huu kuliko wanawake.

Matibabu ya ugonjwa wa Parkinson[hariri | hariri chanzo]

Kwa sasa, hamna matitabu ya kutibu ugonjwa huu lakini kuna dawa ambazo wagonjwa hupewa ili kudhibiti dalili za ugonjwa. Matibabu haya ni kama levodopa na sinemet. Dawa hizi hufanya kazi kwa muda fulani tu na baadaye huwa hazifanyi. Ifikapo kipindi hiki, wagonjwa hushauriwa kula vizuri na kufanya mazoezi ambayo husaidia pia kudhibiti ugonjwa.

Madawa kama levodopa na sinemet husaidia katika kudhibiti mtetemeko, ukosefu wa usingizi, wasiwasi pamoja na dalili nyinginezo za ugonjwa huu.

Suala kuhusu matumizi ya marijuana au bangi iliyotolewa THC (kiungo kinachomfanya mtu alewe anapovuta bangi) yamekuwa yakijadiliwa ikisemekana kwamba cbd oil husaidia katika kudhibiti kiwango cha dopamini mwilini.

Vifaa maalumu vya wagonjwa wa Parkinson[hariri | hariri chanzo]

Kwa sababu ya kutetemeka, pamoja na shida ya kutembea, wagonjwa wa Parkinson huwa na vifaa maalumu ambavyo wanatumia kuwawezesha kumudu maisha. Kwa mfano, kuna vijiko vinavyowasaidia kula chakula hata kama wanatetemeka kwa mikono. Vijiko hivi huenda vikawa na uzito mwingi kuliko vijiko vya kawaida au viwe na teknolojia ya hali ya juu hivi kwamba vinaweza kujua upande ulioko mdomo na kwa hivyo kudhibiti mtetemeko wa mgonjwa hadi atakapokielekeza chakula kwa mdomo. Kuna vikombe pia za kusaidia mgonjwa aweze kunywa kinywaji bila ya kumwagika. Vikombe hivi huundwa kwa muundo utakaoweza kumudu mtetemeko wa mgonjwa wa Parkinson.

Vifaa vingine ni vijiti vya kumsaidia mgonjwa aweze kutembea bila kuanguka kwa kujishikilia kwa ile walker[1].

Watu mashuhuri waliokuwa na ugonjwa wa Parkinson[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Rod of Asclepius2.svg Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ugonjwa wa Parkinson kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.