Nenda kwa yaliyomo

Tungo kirai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tungo kirai ni kipashio kidogo cha kimuundo chenye neno moja au zaidi ambacho hakina muundo wa kiima (K) na kiarifu (A). Kirai huwa na neno kuu moja kinalotawala. Neno hilo linalotawala ndilo huwa/hukupa dhana (aina) ya kirai. mfano. Mtoto yule ni mjinga.

Yule ni mjinga- ni Kirai kivumishi

Uanishaji wa kirai

Uanishaji wa virai umejikita katika aina za maneno, yaani, aina za virai zinatokana na aina za maneno. Kwa kutumia kigezo hicho tunapata aina za virai zifuatazo:

(i) Kirai nomino (KN) (ii) Kirai kivumishi (KV) (iii) Kirai kitenzi (KT) (iv) Kirai kielezi (KE) (v) Kirai kiunganishi (KU) (vi) Kirai kihisishi (KH)

(i) Kirai nomino (KN)

Muundo wa kirai nomino umejikita katika nomino au mahusiano ya nomino. Neno kuu linalotawala muundo huu ni nomino. Kirai nomino kinaweza kuundwa na:

(A) Nomino moja

Mfano:

  • Baba
  • Kalamu
  • Embe
  • Darasa
  • Nyumba
  • Kunguni
  • Tanzania
  • Kenya
  • Uganda
  • Rwanda
  • Burundi
(B) Nomino na nomino

Mfano:

  • Baba na mama
  • Wazee kwa vijana
  • Paka na panya
(C) Kiwakilishi

Hapa unatumia aina zote za viwakilishi Mfano: Wewe, ninyi, mimi, sisi, yeye, wao, n.k.

(ii) Kirai kivumishi (KV)

Kirai kivumishi muundo wake umejikita katika vivumishi. Kirai kivumishi hutawaliwa na aina zote za vivumishi.

Mifano
  • Nyumba 'yetu imebomoka'
  • Kitabu cha mwalimu kimepotea
  • Chakula kitamu kimekwisha

(iii) Kirai kitenzi (KT)

Kwa kuangalia muundo wa Kirai hiki huundwa kwa vitenzi vya aina zote.(Mollel Loserian,kutoka udsm)anasema:

Mifano
  • Cheza
  • Kimbia
  • Ni
  • -Kuwa
  • Soma, n.k.

(iv) Kirai kielezi (KE)

Kirai hiki huundwa kwa aina mbalimbali za vielezi: Mfano:

  • Polepole
  • Sana
  • Mara mbili
  • Asubuhi
  • Darasani, n.k.

(v) Kirai kiunganishi (KU)

Kirai hiki huundwa kwa kutumia viunganishi mbalimbali. Mfano:

  • Ingawa
  • Na
  • Kwa kuwa
  • Bila
  • Pasipo
  • Sembuse
  • Lakini,
  • japokuwa n.k

(vi) Kirai kihisishi (KH)

Kirai hiki huundwa kwa kutumia aina zote za vihisishi. Mfano:

  • Duh!
  • Aisee!
  • Kumbe!
  • Loh!
  • Naam!
  • Ewa!
  • Ahsante!

Tazama pia

Lango:Lugha

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tungo kirai kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.