Trifilo wa Nikosia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Mt. Trifilo.

Trifilo wa Nikosia (Roma, Italia, au Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, mwanzoni mwa karne ya 4Nikosia, Kupro, 370) alikuwa askofu wa mji huo[1].

Baada ya kusoma sheria huko Beirut, Lebanoni[2], aliongokea Ukristo kwa msaada wa Spiridoni wa Tremetusia akasaidia sana kutetea imani sahihi na kupinga teolojia ya akina Ario. Kwa hiyo Atanasi alimsifu.

Maandishi yake [3] yamepotea. Imebaki tu kumbukumbu ya ufasaha wake katika kuhubiri ambao kadiri ya Jeromu ulizidi ule wa wengine wote wa wakati ule[4][5][6][7].

Tangu kale anaheshimiwa na Ukristo wa Mashariki na Ukristo wa Magharibi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Juni[8].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/93027
  2. Sozomeno, Historia Ecclesiastica, I, 11
  3. Jeromu, De viris illustribus, 92.
  4. Orthodox Church in America. "St Triphyllius the Bishop of Leucosia (Nicosia) in Cyprus". Lives of the Saints. Orthodox Church in America. Iliwekwa mnamo March 29, 2013.  Check date values in: |accessdate= (help)
  5. "SAINT TRIPHYLLIUS". St. Nicholas Russian Orthodox Church, McKinney, Texas. Iliwekwa mnamo March 29, 2013.  Check date values in: |accessdate= (help)
  6. "St. Triphyllius, bishop of Leucosia (Nicosia) Cyprus". stjohndc.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-11-01. Iliwekwa mnamo March 29, 2013.  Check date values in: |accessdate= (help)
  7. "St. Triphyllius". Saints and angels. catholic.org. Iliwekwa mnamo March 29, 2013.  Check date values in: |accessdate= (help)
  8. Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.