Nenda kwa yaliyomo

Tongoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tongoni, Tanga)
Magofu ya tongoni
Magofu ya Tongoni, Kata ya Tongoni, Wilaya ya Tanga.

Tongoni ni kata iliyopo ndani ya eneo la Jiji la Tanga katika Mkoa wa Tanga, Tanzania, yenye Postikodi namba 21207.

Kata ina ukubwa wa kilomita za mraba 44 (maili 17),[1] pia ina mwinuko wa wastani wa mita 30 (futi 98)[2].

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 6,103 [3]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,594 [4][5] waishio humo.

Tongoni iko takriban kilomita 14 upande wa kusini wa kitovu cha jiji kando ya barabara inayokwenda Pangani, ikitazama Bahari Hindi.

Katika kata hiyo yanapatikana magofu ya Tongoni, mji wa Waswahili enzi za mawe za kati. Mahali pa kihistoria jinsi inavyoonekana leo kuna msikiti na takriban makaburi 20.[6]

Takriban miaka 600 iliyopita kulikuwepo hapa mji wa Tangata (pia: Mtangata) iliyokuwa mahali muhimu pa biashara. Mahali pake kwenye mdomo mpana wa mto unaoishia hapa palileta nafasi salama ya kutia nanga kwa jahazi. Inasemekana ya kwamba nahodha Mreno Vasco da Gama alipumzika hapa kidogo wakati wa safari yake ya kwanza kuelekea Bara Hindi mnamo mwaka 1498. Magofu ni pamoja na msikiti na makaburi yenye nguzo jinsi ilivyokuwa kawaida kwenye makaburi ya Waswahili.[7]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.citypopulation.de/en/tanzania/northern/admin/
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-06-02. Iliwekwa mnamo 2022-08-12.
  3. https://www.nbs.go.tz
  4. "Sensa ya 2012, Tanga - Tanga CC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-16.
  5. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2022-03-26. Iliwekwa mnamo 2022-08-12.
  6. Tongoni Ruins, tovuti ya Lonely Planet, iliangaliwa Septemba 2018
  7. Briggs, McIntyre ukurasa 372
  • Philip Briggs, Chris McIntyre: Tanzania Safari Guide: With Kilimanjaro, Zanzibar and the Coast, Bradt Travel Guides 2013, ISBN-10: 9781841624624, ISBN-13: 978-1841624624ISBN
Kata za Wilaya ya Tanga - Tanzania

CentralChongoleaniChumbageniDugaKiomoniKirareMabawaMabokweniMagaoniMajengoMakororaMarunguMasiwaniMaweniMnyanjaniMsambweniMwanzangeMzinganiMzizimaNgamiani KaskaziniNgamiani KatiNgamiani KusiniNguvumaliPongweTangasisiTongoniUsagara


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tongoni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.