Teolojia
Teolojia (pia theolojia na thiolojia[1] kutoka maneno ya Kigiriki θέος, theos, "Mungu" + λογία, logia, "usemi") ni elimu juu ya Mungu hasa katika Ukristo. Hiyo haitenganiki na utendaji wake wa nje, yaani uhusiano wake na viumbe vyote.
Jina lingine la fani hiyo lenye asili ya Kiarabu ni Tauhidi. Hilo linatumiwa zaidi na Waislamu. Kwa Kiswahili limetungwa pia jina "Taalimungu".
Basi, ikitajwa kwa jina la mkopo kutoka Kigiriki, fani hiyo inachunguza hasa imani ya Kikristo kadiri ya Ufunuo wa Mungu uliokamilika katika Yesu Kristo na Mitume wake.
Kwa sababu hiyo inategemea hasa Maandiko Matakatifu ya Biblia, lakini pia, kadiri ya madhehebu husika, Mapokeo ya Mitume yasiyoandikwa pamoja na mamlaka hai ya Kristo waliyonayo maaskofu (Ualimu wa Kanisa).
Teolojia hufundishwa katika vyuo na katika nchi mbalimbali; iko pia kama idara ya Chuo Kikuu. Idara hizi mara nyingi zinatenganishwa kimadhehebu. Mtu aliyepita mafundisho ya chuo huitwa mwanateolojia.
Kwa Wakristo maneno ya Yesu mwenyewe, ambayo ni “roho, tena ni uzima” (Yoh 6:63) yana ladha bora kuliko maelezo yote ya teolojia. Lugha ya Injili inatuzamisha katika sala kuliko lugha ya kitaalamu, hata ile yenye hakika ya juu. Inafaa tupumue hewa safi ya vilele hivyo vinavyobubujika maji hai. “Mafundisho ya Yesu Kristo yanapita yale yote ya watakatifu, na mtu aliye na roho yake anakuta humo mana iliyositirika. Lakini inatokea kuwa wengi, kwa kusikia Injili mara nyingi, hawaguswi inavyotakiwa, kwa sababu hawana roho yake. Mnataka kuelewa kwa dhati na kufurahia maneno ya Yesu Kristo? Mjitahidi kulinganisha maisha yenu yote na ya kwake” (Kumfuasa Yesu Kristo I,1:2).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Tahajia "teolojia" ni kawaida katika Kanisa Katoliki, "theolojia" zaidi kati ya Waprotestanti
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- "Theology" on Encyclopædia Britannica
- http://www.theology.ie Ilihifadhiwa 5 Oktoba 2017 kwenye Wayback Machine.
- Chattopadhyay, Subhasis. [1]Reflections on Hindu Theology in Prabuddha Bharata or Awakened India 120(12):664-672 (2014). ISSN 0032-6178. Edited by Swami Narasimhananda.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |