Nenda kwa yaliyomo

Teta Lando

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alberto Teta Lando ( 2 Juni, 1948 [1]14 Julai, 2008 ), alikuwa mwanamuziki wa nchini Angola.[2]

Teta alizaliwa Mbanza Kongo, mji mkuu wa Mkoa wa Zaire kaskazini mwa nchi ya Kongo. Anajulikana sana katika nchi za Kiafrika zinazozungumza Kireno na Ureno yenyewe.

Muziki wake ulilenga utambulisho wa Angola, vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Alizungumza na kuimba kwa lugha zote mbili za Kireno na Kikongo . Miongoni mwa nyimbo zake zilizojulikana sana zilikuwa kama "Irmão ama teu irmão" ("Ndugu, Mpende Ndugu Yako") na "Eu vou voltar" ("Nitarudi").

Katika miaka kadhaa ya mwisho wa maisha yake, aliweza kuunganisha kundi la wanamuziki wengi wa Angola. [3]

Alifariki mjini Paris, Ufaransa, baada ya kuugua saratani .

Orodha ya kazi za muziki

[hariri | hariri chanzo]
  • Memórias 1968-1990 (Teta Lando Produções, Luanda, Angola)
  1. "Archived copy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-09-30. Iliwekwa mnamo 2009-07-17.{{cite web}}: CS1 maint: archived copy as title (link)
  2. "Teta Lando". Discogs (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
  3. "President Dos Santos Praises Singer Teta Lando's Election". www.angolapress-angop.ao. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-08-24. Iliwekwa mnamo 2008-04-15.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Teta Lando kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.