Kikongo
Mandhari
(Elekezwa kutoka Kikoongo)
Kikongo (pia: Kikoongo) ni lugha ya Kibantu inayotumika hasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako inahesabiwa kati ya lugha 4 za taifa. Kinazungumzwa na Wakongo. Idadi ya wasemaji wa Kikongo kama lugha ya kwanza katika Jamhuri hiyo imehesabiwa kuwa watu milioni tatu; pamoja na hayo kuna watu milioni tano ambao huongea Kikongo kama lugha ya pili. Tena kuna wasemaji wa Kikongo milioni moja nchini Angola na milioni moja nchini Jamhuri ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kikoongo iko katika kundi la H10.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- lugha ya Kikoongo kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kikoongo Ilihifadhiwa 3 Julai 2014 kwenye Wayback Machine.
- lugha ya Kikoongo katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/kng
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kikongo kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |