Nenda kwa yaliyomo

Tesistosteroni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tesistosteroni ni aina ya homoni yenye maana sana katika maisha ya mwanamume katika kukua kwa pumbu pamoja na kibofu (prostate). Tofauti ya homoni ya tesistosteroni ni homoni ya estrogeni ambayo inapatikana haswa kwa wamama.

Homoni hii pia husaidia katika kubalehe kwa wavulana ili wawe wanaume katika ukuzi wa mwili, kuwanda kwa mabega, kukua ndevu, kuwa na sauti nzito na pia kuweza kuzaa wanapojamiana na wanawake.

Homoni ya tesistosteroni hupatikana kwa watu wote, waume kwa wake. Hata hivyo kiwango cha homoni hii kwa wanaume huwa mara saba ikilinganishwa na wanawake. Kiwango cha kawaida cha homoni hii huwa kati ya 150 hadi 850 ng/. Vivyo hivyo, wanaume wana homoni ya estrogeni chache ikilinganishwa na wamama.

Mwisho wa uzazi kwa wanaume[hariri | hariri chanzo]

Tesistosteroni hutengenezwa na pumbu na pia katika ubongo wa mwanadamu. Ndio maana wanawake pia huwa na kiwango fulani cha tesistosteroni hata kama hawana pumbu.

Utengenezaji wa homoni hii hupungua pindi mtu anapozeeka. Wanaume wengi walio na umri wa miaka arobaini kwenda juu hupata kwamba kiwango chao chaendelea kudidimia. Hali hii hufanya wasiweze kupata ngono na wake zao maana viungo vyao vya mwili haziwezi kazi hiyo. Kando na hilo, mwananume mwenye upungufu wa homoni hii huwa hana raha, nguvu za kufanya kazi na huonekana kana kwamba ni mlegevu akilinganishwa na mwanaume mwenye tesistosteroni kwa wingi.

Kwa sababu hii, wao huona heri waende kwa daktari ili wajazwe kiwango fulani cha homoni ama wanywe tembe zinazouzwa na makampuni ya. Dawa hizi hujulikana kama steroidi anaboliki. Hata hivyo idara za madawa katika nchi nyingi zimeonya watu wasinywe madawa hayo ya steroidi anaboliki bila idhini ya daktari maana yamepatikana kuwa na madhara baada ya matumizi ya muda mrefu. Hata hivyo, kampuni za madawa ya steroidi zimepitisha steroidi nzuri zilizoidhinishwa na idara ya FDA.

Tesistosteroni husaidia mwanamume awe na uchu wa ngono, awe na misuli iliyotitimka na pia awe mwenye raha akifanya kazi zake .

Wanasayansi wamegundua kwamba mwanamume akiwa na kiwango kingi cha homoni hii na kiwango kidogo cha kotisoli (stress hormone) huwa ana uwezo wa kuongoza watu wakimfuata bila pingamizi yoyote. [1]

Kuongeza tesistosteroni mwilini[hariri | hariri chanzo]

Tesistosteroni huongezewa kwa mwili haswa kwa lishe bora yenye madini ya zinki, magnesium na boron.Chakula kama samaki, oysters na matunda kama ndizi, maembe na parachichi yamesemekana kuongezea madini haya mwilini. Utafiti waonyesha kuwa matawi na mizizi ya stinging nettle husaidia kuongezea homoni ya tesistosteroni.

Madhara ya tesistosteroni nyingi[hariri | hariri chanzo]

Kiwango cha tesistosteroni kikiwa kingi pia huwa na madhara kama vile:

  • kupungua kwa saizi ya pumbu
  • kupata kipara kichwani au nywele kuanguka anguka.
  • wanaume kupata matiti, jambo linalojulikana kama jinekomastia
  • kuwa mwingi wa hasira.
  • chunusi
  • huweza kuzidisha saratani ya kibofu (prostate cancer). Hata hivyo jambo hili halijathibithishwa kwa uhakika.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-29. Iliwekwa mnamo 2017-07-10.

Viungo ya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tesistosteroni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.