Nenda kwa yaliyomo

Steroidi anaboliki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Steroidi anaboliki ni miambatanisho inayohusisha androjeni asili, kama vile tesistosteroni, pamoja na chachu bandia nyingine zinazotengenezwa katika maabara kama ilivyo kwa homoni ya tesistosteroni. Mfano wa steroidi anaboliki ni kama testogeni.

Steroidi huongeza madini ya protini kwa mwili, hasa kwa kutitimua misuli na hutumiwa sanasana na wanamichezo wanaotaka kufanya vizuri katika nyanja za michezo.

Pia hutumiwa na wauguzi kwa kutibu wagonjwa waliokondeana kutokana na magonjwa kama vile Ukimwi na Saratani.

Sababu za kuzitumia

[hariri | hariri chanzo]

Homoni za tesitosteroni hutengenezwa kwa njia asili katika pumbu na pia kwa ubongo wa mtu. Kwa sababu hiyo, waume kwa wake wana tesistosteroni. Hata hivyo wanaume wanapofikisha umri wa miaka arobaini na kwenda juu, kiwango cha homoni kinachotengenezewa mwilini hupungua. Hali hii hufanya mwanamume awe amezembea kwa wakati wote, asiye na raha hata kidogo na pia humpunguzia uchu wa kuonana kimwili na mpenziwe. Mwanamume aliye na homoni hii kwa wingi huwa na nguvu nyingi kazini mwake, raha nyingi na pia ni mwingi wa bashasha kwa wenzake.

Steroidi anaboliki ni za aina tatu kulingana na vile watu wanavyoziingiza mwilini:

  1. Kuna zile za tembe za kumeza kama chakula au tembe za kawaida.
  2. Kuna zile ambazo daktari anakudunga sindano na
  3. Kuna za kupaka ambazo huingia mwilini kupitia ngozi.

Utafiti waonyesha kwamba steroidi anaboliki hazitafanya kazi kama mtu atazitumia bila kupata lishe bora au kufanya mazoezi.

Pia huchukua muda kabla matokeo ya steroidi anaboliki kupatikana kwa wale wanaozitumia.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Steroidi anaboliki zilianza kutengenezwa miaka ya 1930 na zimekuwa zikitumiwa na wanaume wanaotaka kukuza miili haraka.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Wanaotumia steroidi anaboliki huwa wanataka:

  1. kutitimua misuli ili iwe mikubwa.
  2. kuongeza hamu ya ngono au libido.
  3. kuharakisha kubalehe haswa kwa waliochelewa.
  4. kuongezea damu mwilini.
  5. kusawazisha homoni ya testosteroni mwilini.
  6. kuongezea uzani haswa kwa waliokonda kwa maradhi ya Ukimwi au Saratani.
  7. kupunguza mafuta mwilini haswa kwa upande wa kiuno.

Utumiaji mbaya wa steroidi anaboliki

[hariri | hariri chanzo]

Utumiaji wa steroidi anaboliki kwa muda mrefu bila idhini ya muuguzi unaweza kusababisha maafa kama vile: [1]

Kupigwa marufuku

[hariri | hariri chanzo]

Shirika la Kukagua Madawa la Marekani (FDA) limepiga marufuku steroidi anaboliki zozote ambazo hazijafikia viwango ambavyo shirika hilo limeidhinisha. Pia, dawa zozote ambazo zinawaletea madhara wagonjwa zimepigwa marufuku.

Matumizi yake yamepigwa marufuku katika michezo mbalimbali. Vyama vya michezo vinavyokataza wanamichezo wake kutumia steroidi anaboliki ni kama vile World Wrestling Entertainment, National Basketball Association, na National Hockey League.

Dawa za anaboliki steroidi hutengenezwa kwenye maabara za kemikali na dawa. Hata hivyo, katika nchi ambazo zimekataza matumizi yake, inabidi watengenezaji wazitengenezee nyumbani mwao na baadaye kuziuza kinyume cha sheria. 

  1. "Matumizi mabaya ya steroidi anaboliki".

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Steroidi anaboliki kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.