Stefano Nemanja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa ukutani ukimuonyesha Mt. Simeon (Stefan Nemanja), Studenica Monastery.

Stefano Nemanja (kwa Kiserbokroatia: Стефан Немања, stêfaːn ně̞maɲa; Ribnica, 1113 hivi – Monasteri ya Hilandar, 13 Februari 1199) alikuwa mtemi (Veliki Župan) wa Serbia miaka 1166 - 1196.

Ndiye mwanzilishi wa nasaba wa Nemanjić, na anakumbukwa kwa michango yake katika historia na utamaduni wa nchi yake na wa Kanisa lake.[1]

Mwaka 1196 aling'atuka akahamia katika Mlima Athos, awe mmonaki mwenye jina la Simeoni, karibu na mwanae Sava, askofu mkuu wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodoksi la Serbia.

Muda mfupi baada ya kifo chake na miujiza mbalimbali, alitangazwa mtakatifu kwa jina la Свети Симеон Мироточиви.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 100 najznamenitijih Srba. Serbian Academy of Sciences and Arts. 1993. ISBN 86-82273-08-X.; 1st place

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.