Podgorica

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Podgorica nchini Montenegro

Podgorica (Kiserbia: Подгорица tamka pod-go-ri-tsa)ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Montenegro mwenye wakazi 140,000. Iko kwa 42°28′12″N, 19°16′48″E pale ambako mito ya Ribnica na Morača inapokutana. Mji uliitwa Titograd kati ya 1946 hadi 1992.

Mji umejulikana tangu 1326 ulikuwa sehemu ya ufalme wa Serbia. Tangu 1466 ilitawaliwa na Waosmani hadi 1878 wakati Montenegro ilipopata uhuru wake.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia mji ukawa mji mkuu wa jamhuri ya Montenegro ndani ya shirikisho la Yugoslavia. Umeendelea kuwa mji mkuu tangu uhuru wa nchi mwaka 2006.

Picha za Podgorica[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Podgorica kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.