Nenda kwa yaliyomo

Sigebert III

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Sigebati III katika dirisha la kioo cha rangi huko Clichy.

Sigebati III (630 hivi - 1 Februari 656) alikuwa mfalme wa Austrasia kutoka katika familia ya Merovingian kuanzia mwaka 633 mpaka kifo chake kwenye 656.

Alielezewa kama mfalme wa kwanza wa Wafaranki asiyeshughulikia siasa, akimuachia meya wa ikulu atawale wakati wote. Hata hivyo aliishi Kikristo na alijenga monasteri nyingi na kutoa misaada mikubwa kwa makanisa na kwa maskini. [1]

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu, sawa na mwanae Dagobert II.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Februari.[2]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "CatholicSaints.Info » Blog Archive » Butler's Lives of the Saints – Saint Sigebert II, French King of Austrasia, Confessor" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-07-25.
  2. Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.