Samsoni wa Konstantinopoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Samsoni wa Konstantinopoli (kwa Kigiriki: Σαμψὼν ὁ φιλόξενος, Sampsón ho philóxenos; alizaliwa Roma, Italia akafariki Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 530 hivi) alikuwa daktari aliyepata umaarufu kwa huduma yake hata akapewa upadirisho.

Baada ya kumponya kaisari Justiniani I alimuomba kama shukrani amjengee hospitali kwa ajili ya maskini ambayo ilitoa huduma kubwa kwa miaka 600 baadaye[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi, Wakatoliki na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Juni[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.