Nenda kwa yaliyomo

Raga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Rugby)
Tackling ya rugby

Raga (ing. rugby) ni jina la mchezo wa mpira unaochezewa kwa namna mbalimbali na ni aina ya michezo ya timu inayopendwa hasa katika nchi zenye urithi wa utamaduni wa Uingereza kama vile nchi za Jumuiya ya Madola (Australia, Fiji, Samoa, Tonga, Afrika Kusini, Nyuzilandi au Zimbabwe na mengine) na katika nchi kadhaa ina sifa ya kuwa mchezo wa kitaifa (Nyuzilandi, Visiwa vya Cook, Fiji, Samoa, Tonga, Welisi). Nje ya Jumuiya ya Madola mchezo huo ni maarufu Ufaransa, Argentina na Japani.

Rugby ilianzishwa nchini Uingereza sambamba na mpira wa miguu Wakati wa karne ya 19. American Football imezaliwa kutoka kwa rugby ya Kiingereza.

Shabaha ya mchezo ni kubeba au kukanyaga mpira kupitia timu ya wapinzani hadi goli na kuuingiza kwenye goli juu ya mti wa kulala.

Mpira una umbo la duaradufu. Timu mbili ambazo kwa kawaida huwa na wachezaji 15 zinashindana. Mpira unaweza kushikwa kwa mkono; kuna rukhsa kuupa kwa mchezaji mwingine au kuutupa nyuma. Lakini kuutupa mbele ni kosa ndogo unaofuatwa na tendo la "scrum". Hapo mpira unawekwa chini na wachezaji 8 wa kila timu wanashikamana na kusukumana hadi mchezaji mmoja anaweza kushika tena mpira.

Kuna rukhsa kumzuia mchezaji na kumwangusha kwa kumshika nyuma ya msari wa mabega. Tendo hili linaitwa "tackle". Akianguka china anapaswa kuachana na mpira. Wakati mchezaji analala chini wengine hawaruhusiwi kushika mpira kwa mikono.


Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Raga kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.