Reli ya abiria ya Dar es Salaam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Reli ya abiria ya Dar es Salaam ni mfumo wa usafiri katika jiji la Dar es Salaam unaotumia njia za reli zilizopo ndani ya eneo la jiji.[1] Ni mojawapo ya mipango miwili iliyoanzishwa na serikali kurahisisha safari ndani ya jiji na kupunguza msongamano,nyingine pia ni mfumo wa mabasi yaendayo haraka ya Dar es Salaam. Huduma za usafiri zinatolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kuzinduliwa kwake, matumizi ya daladala yalikuwa njia ya pekee ya usafiri wa umma. Safari ya uzinduzi zilifanyika tarehe 29 Oktoba mwaka 2012.[2][3]. Umma uliitaja kama "Gari moshi ya Mwakyembe" kwa heshima ya Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi wakati huo.[4] Huduma zilikabiliwa na matatizo kama hali mbaya ya mabehewa na kukwama kwa injini.[5]

Huduma[hariri | hariri chanzo]

Gari moshi hazipatikani mfululizo siku nzima bali kwenye saa ya asubuhi na jioni pekee. Huduma ya TAZARA inaanza kwenye kituo kikuu kilichopo njiapanda ya Barabara ya Nelson Mandela na Barabara ya Julius K. Nyerere ikiendelea kwa kilomita 30 hadi Mwakanga. Treni za mzunguko husafirishaji abiria 9,000 kila siku lakini hakuna huduma wakati wa Jumapili na kwenye sikukuu. TRC inahudumia njia mbili za jijini[6]. Moja inaunganisha kituo kikuu kwenye Railway Street mjini na Pugu, ikitumia vituo vya Pugu Station, Mwisho wa Lami, Gongo la Mboto, FFU Mombasa, Banana (Njia Panda Segerea), Karakana, Vingunguti Mbuzi, Bakhresa, Kamata na Stesheni. Nyingine iko kati ya kituo kikuu na Ubungo-Maziwa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Dar es Salaam launches first commuter trains", BBC News, 29 October 2012. Retrieved on 3 December 2013. 
  2. MWACHANG`A, DEVOTA. "Dar residents happy with commuter train services", IPP Media, 30 October 2012. Retrieved on 4 December 2013. 
  3. Mtweve, Sturmius. "… Most residents were unaware", 29 October 2012. Retrieved on 4 December 2013. Archived from the original on 2016-03-04. 
  4. Masha, Marycelina. "Dar commuter trains easing transport nightmares", 29 October 2012. Retrieved on 3 December 2013. Archived from the original on 4 December 2013. 
  5. Salum Mihayo: Sustainability of Dar Es Salaam commuter Train in reducing traffic congestion: a case of Tanzania railway limited (TRL) Archived 16 Agosti 2021 at the Wayback Machine., Dissertation Submitted to Mzumbe University, Dar es Salaam Business School in Partial Fulfillment of the Requirements for the Award of Master's of Science Degree in Procurement and Supply Chain Management (PSCM), 2013.
  6. TRL introduces commuter train City Centre - Pugu, Guardian newspaper 04.08.2016