Nenda kwa yaliyomo

Pinocchio (filamu ya 1940)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Pinocchio)
Pinocchio

Posta ya filamu
Imeongozwa na Ben Sharpsteen
Hamilton Luske
Norman Ferguson
T. Hee
Wilfred Jackson
Jack Kinney
Bill Roberts
Imetayarishwa na Walt Disney
Imetungwa na Aurelius Battaglia
William Cottrell
Otto Englander
Erdman Penner
Joseph Sabo
Ted Sears
Webb Smith
Based on the book by Carlo Collodi
Nyota Cliff Edwards
Dickie Jones
Christian Rub
Mel Blanc
Walter Catlett
Charles Judels
Evelyn Venable
Frankie Darro
Imesambazwa na RKO Radio Pictures
Imetolewa tar. Februari 7, 1940 (1940-02-07)
United States
Februari 9, 1940 (1940-02-09)
Ina muda wa dk. 88
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu US$2,289,247
Mapato yote ya filamu $84,254,167[1]

Pinocchio ni filamu ya katuni ya Marekani ya mwaka wa 1940 iliyotayarishwa na Walt Disney na inatokana na hadithi ya Kiitalia ya Carlo Collodi aliyesimulia vituko vya mwanaserere Pinokyo ("Le avventure di Pinocchio"). Kitabu hicho kiliwahi kutafsiriwa na Tanganyika Mission Press kwa Kiswahili mwaka 1965 na kuwa maarufu Afrika Mashariki kwa jina "Mambo yalioyompata Pinokyo".

Hii ni filamu ya pili kutolewa katika mfululizo wa filamu za katuni za Walt Disney, na ilitengenezwa baada ya kupata mafanikio makubwa katika filamu ya awali ya Snow White and the Seven Dwarfs na ilitolewa katika makumbi na RKO Radio Pictures tarehe 7 Februari 1940.

Hadithi ya filamu hii inamhusisha kikaragosi cha mbao anayeitwa Pinocchio (sauti ya Dickie Jones) ameletwa maishani na kichimbakazi cha buluu (Evelyn Venable), ambaye anamweleza kwamba anaweza kuwa kijana wa kweli iwapo atajibitisha kama ni "jasiri, mkweli, na si mchoyo". Hivyo kikaragosi huyo anaianza safari ili ili awe kijana wa kweli, ambamo kunatokea mashambulizi mengi wakati wa safari hiyo.

Ndani yake wanakuja Aurelius Battaglia, William Cottrell, Otto Englander, Erdman Penner, Joseph Sabo, Ted Sears, na Webb Smith kutoka katika kitabu cha Collodi. Matayarisho yake yalisimamiwa na Ben Sharpsteen na Hamilton Luske, na mfululizo wa filamu uliongozwa na Norman Ferguson, T. Hee, Wilfred Jackson, Jack Kinney, na Bill Roberts.

Tazama pia

Marejeo

  1. "Pinocchio". Box Office Mojo. Iliwekwa mnamo 2009-06-10.

Viungo vya Nje