Tarzan (filamu ya 1999)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tarzan ni filamu ya mwaka 1999 iliyodhaminiwa na Walt Disney Features Animations kwa ajili ya Walt Disney Pictures. Inahusu historia ya Tarzan of the Apes iliyotolewa na Edgar Rice Burroughs. Filamu hii inahusu mtoto mdogo aliyelelewa na kundi la sokwe walio msituni baada ya mtoto wao wa halisi kuliwa na chui. Katika katuni hii mtoto huyu anarithishwa jina la Tarzan. Tarzan amekuwa akiishi vizuri na wanyama wengine wote bila ya kujua kuwa baba yake bandia ambaye ni sokwe alimchukia kwa sababu ya kuwa Tarzan siyo mtoto wake wa halisi.madhumuni makuu ya filamu hii yanaanza ambapo Tarzan anakutana na msichana anayetokea mjini pamoja na baba yake na mlinzi wao .Baada ya Tarzan kukutana na binti huyo ndipo anapoanza kujifunza zaidi maisha ya mjini. Hapa ndipo Tarzan ana gundua ya kwamba yeye si kizazi cha sokwe bali ni kizazi cha binadamu. Lakini baadaye wanakuja kugundua ya kwamba mlinzi wa yule binti ana njama za kuteka wanyama wa msituni pamoja na kumteka Tarzan pia. Lakini Tarzan anajaribu kila anachokiweza na kwa ushirikiano wa binti yule na baba yake pamoja na wanyama wengine Tarzan anafanikiwa kumshinda yule mlinzi na kuhakikisha usalama wa wanyama wote wa msituni.

Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tarzan (filamu ya 1999) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.