Petro wa Narbone

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Petro wa Narbone (Narbonne, Ufaransa - Yerusalemu, leo kati ya Israeli na Palestina, 14 Novemba 1391) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo, padri na mmisionari katika Nchi takatifu ya Yesu.

Kabla hajaenda huko aliishi miaka 15 katika makao ya upwekeni ya Brogliano (Italia).

Alitangazwa na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri mwaka 1889, halafu na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu tarehe 21 Juni 1970.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mfiadini pamoja na Nikola Tavelic, Deodato wa Ruticinium na Stefano wa Cuneo.

Sikukuu yao ni tarehe waliyouawa na Waislamu waliowahubiria Injili[1].

Ua wa monasteri ya zamani ya Mlima Sayuni huko Jerusalem, alipoishi.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • D. Mandić: Documenta martyrii beati Tavelic, Dissertation Gregorianae, Roma 1958.
  • A. Crnica, Historico-iuridica dilucidatio vitae, martyrii et gloriae beati N. Tavelic, Dissertation Gregorianae, Roma 1958,
  • Odilo Lechner, Ulrich Schütz: Mit den Heiligen durch das Jahr. Herder, Freiburg/B. 1988, ISBN 3-451-20485-1, S. 228.
  • Vera Schauber, Hanns Michael Schindler: Heilige und Namenspatrone im Jahreslauf. Pattloch, Augsburg 2001, ISBN 3-629-01642-1, S. 587.
  • Josef Gelmi u.a.: Lexikon der Namen und Heiligen. Edition Nikol, Hamburg 2002, ISBN 3-933203-63-5, S. 609.
  • Ordo Fratrum Minorum: Franziskanisches Proprium. Die Feier des Stundengebetes. Herder, Freiburg/B. 1987, S. 372–375.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  1. Martyrologium Romanum