Deodato wa Ruticinium
Mandhari
Deodato wa Ruticinium au Diode Aribert (labda Rodez, Ufaransa 1340 hivi - Yerusalemu, leo kati ya Israeli na Palestina, 14 Novemba 1391) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo, padri na mmisionari kwanza Bosnia, halafu katika Nchi takatifu ya Yesu.
Pamoja na wenzake Nikola Tavelic, Stefano wa Cuneo na Petro wa Narbone, alichomwa moto kwa kuwa walihubiri hadharani kwa ushujaa dini ya Kikristo mbele ya Waislamu, wakimkiri kwa uimara Kristo Mwana wa Mungu [1].
Pamoja nao alitangazwa na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri mwaka 1889, halafu na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu mfiadini tarehe 21 Juni 1970.
Sikukuu yao ni tarehe waliyouawa na Waislamu waliowahubiria Injili[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- D. Mandić: Documenta martyrii beati Tavelic, Dissertation Gregorianae, Roma 1958.
- A. Crnica, Historico-iuridica dilucidatio vitae, martyrii et gloriae beati N. Tavelic, Dissertation Gregorianae, Roma 1958,
- Odilo Lechner, Ulrich Schütz: Mit den Heiligen durch das Jahr. Herder, Freiburg/B. 1988, ISBN 3-451-20485-1, S. 228.
- Vera Schauber, Hanns Michael Schindler: Heilige und Namenspatrone im Jahreslauf. Pattloch, Augsburg 2001, ISBN 3-629-01642-1, S. 587.
- Josef Gelmi u.a.: Lexikon der Namen und Heiligen. Edition Nikol, Hamburg 2002, ISBN 3-933203-63-5, S. 609.
- Ordo Fratrum Minorum: Franziskanisches Proprium. Die Feier des Stundengebetes. Herder, Freiburg/B. 1987, S. 372–375.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |