Nyigu kidusia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyigu kidusia
Majike ya Megarhyssa macrurus wakionyesha neli zao ndefu za kutagia mayai.
Majike ya Megarhyssa macrurus wakionyesha neli zao ndefu za kutagia mayai.
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Gerstâcker, 1867
Ngazi za chini

Nusuoda 2, familia 61:

Nyigu vidusia ni nyigu ambao lava wao huishi ndani au juu ya arithropodi hai na kujilisha kwa hemolimfu na tishu zao. Kidusiwa anakufa hatimaye. Isipokuwa spishi za familia Pompilidae, zinazodusa buibui, nyigu hao hudusa wadudu wengine. Mara nyingi hubobea spishi moja au labda spishi kadhaa zinazohusiana au vinginevyo familia moja ya wadudu. Viwavi na mabuu ya mbawakawa, nzi na kunguni-mgunda huduswa sana. Siku hizi hutumiwa sana katika udhibiti wa kibiolojia wa wasumbufu wa kilimo.

Nyigu hao wanaweza kugawanywa kulingana na hatua ya maendeleo wanayoshambulia au mkakati wao wa udusio. Kwa hivyo wao ni au endoparasites (kidusia wa ndani), yaani, mabuu hujilisha na kukua ndani ya wadusiwa wao, au ectoparasites (kidusia wa nje), yaani, mabuu hula wadusiwa wao kutoka nje. Nyigu wa kiendoparasitiki wanaweza kushambulia mayai, lava, mabundo au wapevu, ingawa wadusia waa mayai na lava ni kawaida zaidi. Mara nyingi huruhusu kidusiwa wao kuendelea na maendeleo yake, ikiwa ni pamoja na ubambuaji. Nyigu hawa wanaitwa koinobionti. Nyigu wengine ni idiobionti na mabuu yao huishi nje ya wadusiwa wao, ambao ni lava wa wadudu au buibui katika kisa cha bunzi-buibui. Kwa sababu hiyo, wadusiwa hawa wamepooza na jike mpevu kabla ya kuweka yai, ili kidusiwa hawezi kujaribu kuondoa kidusia.

Trissolcus sp. akishamhbulia mayai ya Chinavia sp.

Vidusia wa mayai, ambao kwa hakika ni wadogo sana, kwa kawaida huua kiinitete cha kidusiwa kabla aweze kuibuka. Kinachojitokeza kutoka kwa yai ni kidusia mpevu, hivyo hatua zote za maendeleo zimetokea ndani ya yai. Wadusia wa lava huruhusu kidusiwa kukuza na kubambua kwa kulisha tishu zisizo muhimu. Wakubwa zaidi wanaweza kuibuka kutoka kwa bundo badala yake. Nyigu wengine hushambulia wadusiwa, kwa kawaida viwavi, ambao ni wakubwa sana kuliko wao wenyewe na hutaga idadi ya mayai ndani yao. Kwa hivyo, mabuu mengi hutoka katika hatua ya mwisho ya kiwavi.

Udhibiti wa kibiolojia[hariri | hariri chanzo]

Nyigu vidusia hufikiriwa kuwa na manufaa kwani kwa asili hudhibiti idadi za wadudu waharibifu wengi. Wanatumika sana kibiashara kwa udhibiti wa kibiolojia, ambayo vikundi muhimu zaidi ni Ichneumonidae ambao hushambulia hasa viwavi wa vipepeo na nondo, Braconidae ambao hushambulia viwavi na aina mbalimbali za wadudu wengine ikiwa ni pamoja na vidukari, na Chalcidoidea ambao hudusa mayai na lava wa vidukari, vidung'ata, viwavi wa kabichi na wadudu-gamba[1]. Nyigu vidusia wengine wamewasilishwa kutoka nje ya nchi ili kudhibiti wadudu shambani, kama Apoanagyrus lopezi ili kudhibiti kidung'ata wa muhogo, Phenacoccus manihoti, barani Afrika.[2].

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Parasitoid Wasps (Hymenoptera)". University of Maryland. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-27. Iliwekwa mnamo 6 June 2016.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Cassava mealybug".