Bunzi-buibui

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bunzi-buibui
Bunzi-buibui akivuta bui-nyani (Hemipepsis sp.)
Bunzi-buibui akivuta bui-nyani (Hemipepsis sp.)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba sana)
Familia ya juu: Pompiloidea
Familia: Pompilidae
Latreille, 1805
Ngazi za chini

Nusufamilia 4, jenasi 33 katika Afrika ya Mashariki:

Bunzi-buibui ni nyigu wa familia Pompilidae walio na kiuno chembemba na kirefu sana (petiole). Ingawa spishi fulani za bunzi wengine hukamata buibui, Pompilidae ni familia pekee ambayo spishi zote wanatumia buibui kama chakula cha mabuu yao.

Nyigu wa familia Sphecidae na wa nusufamilia Eumeninae katika familia Vespidae huitwa bunzi pia.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Bunzi-buibui wana kiuno chembamba na kirefu. Spishi kadhaa ni kubwa kabisa ya oda ya Hymenoptera na hufikia zaidi ya sm 5. Urefu wa spishi nyingine ni sm 1-2.5. Metatoraksi imeunganishwa kwa pronoto na mesotoraksi, ili nyigu hao huruka hewani vizuri sana. Juu ya hayo, protoraksi ni imara sana, kwa sababu huchimba na miguu yao ya mbele. Wana miguu mirefu yenye miiba na tibia za nyuma ni ndefu, mara nyingi mpaka kutosha kupitia ncha ya fumbatio. Tibia za nyuma huwa na mwiba unaoonekana vizuri kwenye ncha ya nyuma. Takriban spishi zote zina mabawa marefu, lakini spishi chache zinajulikana ambazo zina mabawa mafupi au hazina mabawa. Kwa kawaida bunzi-buibui ni weusi au buluu iliyoiva, mara nyingi wenye mng'ao wa metali. Walakini, kuna spishi nyingi zilizo rangi kali.

Mwenendo[hariri | hariri chanzo]

Wapevu wa bunzi-buibui hula mbochi ya mimea mbalimbali. Maua fulani hutegemea sana uchavushaji na bunzi-buibui, k.m. gugu-maziwa Pachycarpus asperifolius (jamaa ya mkoe) wa Afrika Kusini[1]. Kulingana na jenasi na spishi bunzi-buibui hukamata spishi nyingi za buibui kama chakula cha mabuu yao wakifunika karibu familia zote za buibui, pamoja na tarantula, bui-nyani, buibui-mbweha, buibui wawindaji na buibui warukaji, ingawa kila mmoja wa bunzi-buibui hushambulia idadi ndogo tu ya spishi za buibui.

Nyigu wa kike akipata buibui humdunga na kumpoozesha. Kwa kawaida buibui aliyelengwa hawezi kuua nyigu, kwa sababu nyigu anaweza kuruka ili kuzuia miguu na kelisera za buibui, kwa hivyo huyu hupambana vikali ili kutoroka[2]. Bunzi-tarantula hawashambulii wakati tarantula wapevu wako karibu na au ndani ya vishimo vyao. Badala ya hiyo nyigu hutafuta madume wapevu ambao wameacha vishimo vyao kutafuta majike kwa kupandana nao. Kwa wazi nyigu kwanza hutumia mabawa yake kupiga hewa juu ya tarantula akimdanganya kufikiria kuwa analengwa na ndege na kwa hivyo tarantula huitika kwa kujikunja ili kuwa mdogo zaidi na kutokuonekana sana, ambayo halafu hufanya tarantula asiweze kujitetea dhidi ya shambulio la nyigu.

Mara tu buibui amepooza, jike hufanya kishimo na hubeba au kuvuta buibui kuelekea hiki au kwenye kishimo kilichofanywa hapo awali[3]. Takriban nyigu hao wote huishi peke yao na kwa hivyo majike hawachimbi vishimo karibu na kila kimoja. Kwa sababu ya saizi kubwa ya mwili wa mawindo yao, bunzi-tarantula hutengeneza vishimbo karibu na mahali pa shambulio au kutumia kishimo au handaki la mawindo. Kwa kawaida bunzi-buibui huwapatia kila mmoja wa mabuu yao mawindo / kidusiwa mmoja ambaye lazima iwe mkubwa ili kutosha kutumika kama chanzo cha chakula wakati wote wa ukuaji wa buu. Kwa kawaida yai moja hutagwa juu ya fumbatio ya buibui na kishimo kufungwa ili buu akue bila kuvurugwa na vidusia au matopasi[3]. Nyigu wa kike anaweza sasa kueneza mchanga au kufanya mabadiliko mengine kwa eneo hilo akiacha mahali pa kishimbo hakionekani.

Yai hutoa buu na huyu hula buibui akivunja kiwambo cha nje kwa mandibuli yake. Buu akila kidusiwa wake huokoa mpaka mwishowe ogani muhimu kama vile moyo na mfumo mkuu wa neva. Kwa kungojea hadi hatua ya mwisho ya ukuaji anahakikisha buibui haitaoza kabla ya buu hajakua kikamilifu[4]. Mabuu wana hatua tano kabla ya kuwa bundo. Tofauti kubwa ya mofolojia hazibainika kati ya hatua nne za kwanza isipokuwa saizi. Hatua ya mwisho ikikamilishwa mabuu husuka kifukofuko cha hariri cha kudumu na huibuka kama wapevu baadaye katika msimu huo huo au kukaa ndani wakati wa msimu wa baridi kulingana na spishi na wakati wa mwaka buu awe bundo[5].

Ceropalinae fulani hutaga mayai yao kwenye buibui anayokiakia bado. wakimpoozesha kwa muda mfupi, na baada ya kutoka katika mayai mabuu ya nyigu hujilisha nje kwa kufyonza hemolimfi. Baada ya muda buibui atakufa na kisha buu aliyekomaa atakuwa bundo. Spishi nyingine hutaga mayai kwenye buibui waliopoozeshwa na bunzi-buibui wengine (kleptoparasitism au udusio baada ya wizi).

Ukubwa wa kidusiwa anaweza kuathiri kama yai la nyigu litaendelea kuwa dume au jike. Mawindo makubwa mara nyingi hutoa majike[6]. Pepsis thisbe wa kusini magharibi mwa Merikani anaonyesha uwiano wa moja kwa moja kati ya urefu wa mwili wa nyigu mpevu na uzito wa buibui kidusiwa, Aphonopelma echina. Kwa sababu saizi ya mpevu wa P. thisbe imedhamiriwa na saizi ya kidusiwa aliyepewa na mama yake, marudio ya saizi za vidusiwa kupitia misimu yataamua ubadilifu wa ukubwa baina ya nyigu wapevu[7].

Kuhusu tabia ya kupandana, madume hupata maeneo ya kukaa ili kutafuta majike walio tayari kwa kupandana na wanaopita. Katika utafiti juu ya bunzi-tarantula Hemipepsis ustulata[8], madume wakubwa wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata maeneo ya kukaa na madume walio na eneo kama hili wanaonekana kuongeza nafasi zao za kupandana kwa sababu majike walio tayari huruka kuelekea mahali pa kukaa panaposhikiliwa na madume hao.

Spishi za Afrika ya Mashariki[9][hariri | hariri chanzo]

 • Anoplius aethiopicus
 • Anoplius bifasciatus
 • Anoplius fuscus
 • Anoplius subfasciatus
 • Anoplius successor
 • Arachnospila consobrina
 • Arpactomorpha pulchella
 • Atopopompilus jacens
 • Auplopus aenescens
 • Auplopus anomalus
 • Auplopus basilewskyi
 • Auplopus brownei
 • Auplopus cameronis
 • Auplopus carinigenus
 • Auplopus cinnamomeus
 • Auplopus commendabilis
 • Auplopus demissus
 • Auplopus domesticus
 • Auplopus enodans
 • Auplopus gemella
 • Auplopus gowdeyi
 • Auplopus imperfectus
 • Auplopus ineptus
 • Auplopus infantulus
 • Auplopus kilimandjaroensis
 • Auplopus lacustris
 • Auplopus laevigatus
 • Auplopus nigeriensis
 • Auplopus ondontocephalus
 • Auplopus perplexus
 • Auplopus planiusculus
 • Auplopus ruficoxa
 • Auplopus ruficinctus
 • Auplopus sansibaricus
 • Auplopus seminitidus
 • Auplopus stigmalis
 • Auplopus subpetiolatus
 • Auplopus sylviculus
 • Auplopus ugandensis
 • Auplopus xanthospilus
 • Batozonellus gowdeyi
 • Batozonus capensis
 • Ceropales africana
 • Ceropales cribrata
 • Ceropales dayi
 • Ceropales ferrugo
 • Ceropales kriechbaumeri
 • Cordyloscelis ugandensis
 • Cryptocheilus rhodesianus
 • Cryptocheilus vittatus
 • Cyemagenia imitatrix
 • Cyemagenia rubrozonata
 • Cyemagenia ugandensis
 • Cyphononyx anguliferus
 • Cyphononyx antennata
 • Cyphononyx optimus
 • Cyphononyx pan
 • Cyphononyx usambarensis
 • Dichragenia pulchricoma
 • Dipogon ugandensis
 • Elaphrosyron multipictus
 • Episyron crassicornis
 • Hemipepsis ascensoi
 • Hemipepsis commixta
 • Hemipepsis dedjas
 • Hemipepsis gestroi
 • Hemipepsis heros
 • Hemipepsis heteroneura
 • Hemipepsis iodoptera
 • Hemipepsis latirostris
 • Hemipepsis mashonae
 • Hemipepsis obscurus
 • Hemipepsis refulgens
 • Hemipepsis rufofemoratus
 • Hemipepsis tamisieri
 • Hemipepsis variabilis
 • Hemipepsis vespertilio
 • Hemipepsis vestitipennis
 • Hemipepsis viridipennis
 • Homonotus aegyptiacus
 • Homonotus rukwaensis
 • Homonotus sansibaricus
 • Java atropos
 • Java caroliwaterhousi
 • Java nigricornis
 • Marimba elgonensis
 • Masisia fasciatipennis
 • Micragenia nubilipennis
 • Paraclavelia anomala
 • Paraclavelia brevipennis
 • Paraclavelia somalica
 • Paracyphononyx affinis
 • Paracyphononyx africanus
 • Paracyphononyx difficilis
 • Paracyphononyx diversus
 • Paracyphononyx frustratus
 • Paracyphononyx lukombensis
 • Paracyphononyx mombassicus
 • Paracyphononyx rotundinervis
 • Parapompilus angustiventris
 • Paraspilotelus fasciatipennis
 • Pezopompilus truncatipennis
 • Platyderes chalybeus
 • Poecilagenia braunsi
 • Poecilagenia nigeriensis
 • Priocnemis albolineatus
 • Priocnemis angustiventris
 • Priocnemis connectens
 • Priocnemis fuscofasciatus
 • Priocnemis inermis
 • Priocnemis iterabilis
 • Pseudopedinaspis marshalli
 • Pygmachus umbratus
 • Tachypompilus praepotens

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. A. Shuttleworth & S. D. Johnson (2006) Specialized pollination by large spider-hunting wasps and self-incompatibility in the African milkweed Pachycarpus asperifolius. International Journal of Plant Science, 167 (6): 1177-1186.
 2. https://www.iflscience.com/plants-and-animals/death-match-tarantula-vs-wasp/
 3. 3.0 3.1 Spider Wasps Australian Museum Online
 4. Punzo, F (2005). "Studies on the natural history, ecology, and behavior of Pepsis cerberus and P. mexicana (Hymenoptera: Pompilidae) from Big Bend National Park, Texas". Journal of the New York Entomological Society 113 (1): 84–95. doi:10.1664/0028-7199(2005)113[0084:sotnhe]2.0.co;2. 
 5. Daly, Howell V.; Doyen, John T.; Purcell, Alexander H. (1998). Introduction to Insect Biology and Diversity. Oxford: Oxford UP. ISBN 978-0-19-510033-4. 
 6. "Spider predators and parasites". Iziko Museums of Cape Town: museums.org.za. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-17. Iliwekwa mnamo 28 November 2006.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |accessdate= (help)
 7. Punzo, F (1994). "The biology of the spider wasp, Pepsis thisbe (Hymenoptera: Pompilidae) from Trans Pecos, Texas. I. Adult morphometrics, larval development and the ontogeny of larval feeding patterns". Psyche 101 (3–4): 229–242. doi:10.1155/1994/70378.  Unknown parameter |doi-access= ignored (help)
 8. Alcock, J.; Kemp, J. (2006). "The behavioral significance of male body size in the Tarantula Hawk Wasp Hemipepsis ustulata (Hymenoptera: Pompilidae)". Ethology 112 (7): 691–698. doi:10.1111/j.1439-0310.2006.01204.x. 
 9. [1] Archived 9 Julai 2021 at the Wayback Machine. Tovuti ya nyigu wa Afrika