Nyambono

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyambono ni kata ya Wilaya ya Musoma Vijijini katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31216.

Kata ya Nyambono inapakana na wilaya ya Bunda kwa upande wa mashariki, kata ya Suguti kwa upande wa kaskazini, Nyamlandilila kwa upande wa magharibi na Bugwema kwa upande wa kusini.

Kata ya Nyambono inaundwa na vijiji vya Bugoji, Nyambono, Kanderema, Kaburabura na Saragana ambapo ndipo makao makuu ya kata.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 11,993 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,106 waishio humo.[2] Sensa ilionyesha kuwa Nyambono ina idadi ya watu 18,106: wanaume 8,888 na wanawake 9,218.

Wenyeji wa kata hii ni Wajita nao wanatunza tamaduni zao za asili zinazolinda maadili ya Mtanzania.

Shughuli za kiuchumi za wakazi ni kilimo cha mazao ya chakula na ya biashara kama vile pamba, mahindi n.k. Pia wanajishughulisha na biashara ndogondogo.

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na upatikanaji wa mawasiliano ya simu kama vile Airtel na Vodacom.

Kuna usafiri wa kila siku wa kwenda na kurudi Bunda Mjini.

Pia kuna zahanati ambayo hivi karibuni imepandishwa hadhi kuwa kituo cha afya.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Musoma Vijijini - Mkoa wa Mara - Tanzania

Bugoji | Bugwema | Bukima | Bukumi | Bulinga | Busambara | Bwasi | Etaro | Ifulifu | Kiriba | Makojo | Mugango | Murangi | Musanja | Nyakatende | Nyambono | Nyamrandirira | Nyegina | Rusoli | Suguti | Tegeruka


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyambono kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.