Nyakatende

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyakatende ni kata ya Wilaya ya Musoma Vijijini katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31203.

Kata hiyo inaundwa na vijiji vya Kigera, Kamguruki, Kakisheri na Nyakatende.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 15,262 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi takriban 19,341 waishio humo.

Wenyeji wa kata hii ni Wakwaya ambao shughuli zao kuu za kiuchumi ni kilimo cha mazao ya mihogo na mahindi.

Waishio karibu na ziwa Viktoria hujishughulisha na uvuvi wa samaki pia.

Uchimbaji wa madini ya dhahabu ni miongoni mwa shughuli zinazoendelea katika kata ya Nyakatende. Machimbo ya Ekungu mine ndipo wachimbaji wakubwa na wadogo wanapopatikana na katika maeneo mbalimbali katani humo biashara nazo zimekua na kuongeza pato la mwananchi.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Musoma Vijijini - Mkoa wa Mara - Tanzania

Bugoji | Bugwema | Bukima | Bukumi | Bulinga | Busambara | Bwasi | Etaro | Ifulifu | Kiriba | Makojo | Mugango | Murangi | Musanja | Nyakatende | Nyambono | Nyamrandirira | Nyegina | Rusoli | Suguti | Tegeruka


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyakatende kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.