Nindi
Nindi ni kijiji ambacho kinapatikata kata ya Lupingu, tarafa ya Mwambao, Wilaya ya Ludewa, mkoa wa Njombe, Tanzania. Ni kama km 20 toka yalipo makao makuu ya wilaya.
Kina jumla ya vitongoji vinne ambavyo ni Nindi Juu, Nindi Kati, Ipombo/Chapwela, na Nindi Chini/Njelela/Mdoleke.
Kijiji cha Nindi kina wakazi zaidi ya elfu mbili kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, ambapo asilimia kubwa ni kutoka kabila la Wakisi, na makabila mengine ni wahamiaji na watumishi wa taasisi mbalimbali.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Kijiji cha Nindi kimepakana na Ludewa/Mlima Ngiru kwa upande wa mashariki, upande wa magharibi imepakana na ziwa Nyasa/nchi ya Malawi, upande wa kaskazini kinapakana na kijiji cha Ntumbati na Lupingu, na upande wa kusini ni kata zaa Iwela na Mkomang'ombe kupitia Mto Ukenju.
Shughuli za kijamii
[hariri | hariri chanzo]Kwa kiasi kikubwa kijiji cha Nindi wananchi wake wanajishughulisha na kilimo na uvuvi na kiasi kidogo ni wafugaji. Wanakijiji wanategemea sana ziwa Nyasa ili kujipatia kipato chao, wakivua samaki wa aina mbalimbali ambao wanauzwa katika soko la wilaya ya Ludewa na kiasi kidogo hupelekwa kwenye masoko ya mbali kama Songea na Dar es Salaam. Mazao yanayolimwa ni mihogo ambayo ni chakula kikuu, mahindi, maharage, viazi vitamu, mbocho/choroko, magimbi, ulezi, mtama, mayautoli.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nindi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |