Nenda kwa yaliyomo

Nikola wa Antiokia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa ukutani wa Fra Angelico, ukionyesha Mtume Petro akiweka wakfu wainjilisti saba wa kwanza.

Nikola wa Antiokia ni Mkristo wa karne ya 1 anayejulikana hasa kutokana na Matendo ya Mitume.

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa na Kanisa Katoliki na Anglikana tarehe 28 Julai pamoja na wenzake Prokoro, Nikanori, Timone na Parmena [1][2].

Mtu wa Antiokia wa Syria, leo nchini Uturuki, alikuwa ameongokea Uyahudi kutoka Upagani. Halafu alijiunga na Ukristo akawa mmojawapo kati ya wanaume saba wa lugha ya Kigiriki katika Kanisa mama la Yerusalemu ambao, wakiwa wamejaa Roho Mtakatifu na hekima, walichaguliwa na waumini wenzao wakawekewa mikono na Mitume wa Yesu ili kushughulikia kwa niaba yao huduma za fukara (Mdo 6)[3].

Irenei wa Lyon anasimulia[4] kwamba ndiye aliyeanzisha uzushi wa Wanikola unaolaaniwa na Ufunuo wa Yohane (2:6,15), lakini Eusebi wa Kaisarea alikanusha habari hiyo[5].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Martyrologium Romanum", Typis Vaticanis, Editio Altera, 2004
  2. Calendar of saints (Episcopal Church in the United States of America)
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/91953
  4. Adversus haereses I, 26
  5. Storia Ecclesiastica, III, 29