Parmena mwinjilisti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mchoro wa ukutani wa Fra Angelico, ukionyesha Mtume Petro akiweka wakfu wainjilisti saba wa kwanza.

Parmena mwinjilisti (alifariki 98) ni Myahudi wa karne ya 1 anayejulikana hasa kutokana na Matendo ya Mitume.

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa na Kanisa Katoliki na Anglikana tarehe 28 Julai[1][2].

Katika Biblia[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa mmojawapo kati ya wanaume saba wa lugha ya Kigiriki katika Kanisa mama la Yerusalemu waliochaguliwa kushughulikia mafukara kwa niaba ya Mitume wa Yesu (Mdo 6).

Katika mapokeo[hariri | hariri chanzo]

Mapokeo ya baadaye yanasimulia kwamba aliinjilisha Asia Ndogo, alikuwa askofu wa Soli, akafia dini yake katika dhuluma ya kaisari Trajan.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Martyrologium Romanum", Typis Vaticanis, Editio Altera, 2004
  2. Calendar of saints (Episcopal Church in the United States of America)
Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Parmena mwinjilisti kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.