Nicolaus Copernicus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Taswira ya Nicolaus Copernicus (mwanzo wa karne ya 16)

Nicolaus Copernicus (kwa Kipolandi: Mikołaj Kopernik; kwa Kijerumani Nikolas Koppernigk, *19 Februari 147324 Mei 1543) alikuwa mtaalamu aliyefaulu kutetea na kueneza fundisho la Aristarko wa Samo kwamba dunia inazunguka jua, kinyume cha fundisho lilotawala awali kuwa jua linazunguka dunia.

Alizaliwa Toruń, mji wa Hansa huko Poland, katika familia yenye damu ya Kijerumani.

Alisoma teolojia, sheria na tiba huko Poland na Italia, akawa |padri wa Kanisa kuu la Frauenburg-Fromburg, ambapo mwaka 1543 alifariki akazikwa chini ya sakafu yake.

Kidogo tu kabla hajafa alitoa kitabu chake "De revolutionibus orbium coelestium" (kuhusu mizunguko wa magimba ya angani), ambacho kina mafundisho makuu ya sayansi ya nyota ya siku hizi, kama vile mpangilio wa sayari na mzunguko wa kila siku wa dunia juu yake yenyewe.

Hata hivyo mafundisho yake yalikuwa na kasoro zilizojulikana baadaye kwa maendeleo ya utafiti: k.mf. alidhani mizunguko ya sayari kandokando ya jua ni ya duara kabisa.

Mafundisho yake yaliongoza wanasayansi wengine kama Galileo Galilei na Kepler, ambao waliyathibitisha na kuyaboresha.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]


About De Revolutionibus
Legacy
German-Polish Cooperations
Scientist.svg Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nicolaus Copernicus kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.