Musa wa Roma
Mandhari
Musa wa Roma (alifariki Roma, Italia, 251) alikuwa padri wa Roma ya Kale aliyeongoza jimbo baada ya kifodini cha Papa Fabiani wakati wa dhuluma ya kaisari Decius.
Aliona vema kupatanisha na Kanisa wale ambao waliwahi kukana imani ya Kikristo na kwa wakati huo walikuwa wagonjwa na katika hatari ya kufa. Akikaa gerezani muda mrefu aliwafariji mara nyingi kwa kuwashirikisha maneno ya barua za Sipriani mfiadini, askofu wa Karthago [1].
Hatimaye akafa gerezani [2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Novemba[3].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |