Upatanishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Upatanishi ni mchakato maalum wa kimuingiliano ambapo mtu wa tatu asiye na upendeleo husaidia pande zinazozozana kusuluhisha migogoro kwa kutumia mbinu maalum za mawasiliano na mazungumzo. Washiriki wote katika upatanishi huimizwa kushiriki kikamilifu katika mchakato. Upatanishi ni mchakato unaozingatia pande zote kimsingi hulenga mahitaji, haki, na maslahi ya wahusika. Mpatanishi hutumia mbinu mbalimbali ili kuongoza mchakato katika mwelekeo chanya na kusaidia pande zenye mgogoro kupata suluhisho lao mwafaka. Mpatanishi ni mwezeshaji kwa kuwa anasimamia mwingiliano kati ya wahusika na kuwezesha mawasiliano ya wazi.

Upatanishi, kama inavyotumika katika sheria, ni njia mbadala ya utatuzi wa mizozo baina ya pande mbili au zaidi yenye athari madhubuti. Kwa kawaida, mtu wa tatu, mpatanishi, husaidia wahusika kujadili suluhu. Wapinzani wanaweza kusuluhisha mizozo katika nyanja mbalimbali, kama vile masuala ya kibiashara, kisheria, kidiplomasia, mahali pa kazi, jumuiya na familia.

Neno upatanishi kwa ujumla linarejelea tukio lolote ambalo mtu wa tatu huwasaidia wengine kufikia makubaliano. Zaidi hasa, upatanishi una muundo, ratiba, na mienendo ambayo katika mazungumzo ya "kawaida" hukosekana. Mchakato huwa  wa faragha na wa siri, ikiwezekana unatekelezwa na sheria. Kwa kawaida ushiriki huwa kwa hiari. Mpatanishi huwa kama mhusika wa tatu asiyeegemea upande wowote na kuwezesha badala ya kuelekeza mchakato. Upatanishi unakuwa suluhisho la kumamilza mzozo kwa  amani zaidi  na linalokubalika kimataifa.  Upatanishi unaweza kutumika kutatua mizozo katika  ukubwa wowote.