Nenda kwa yaliyomo

Nile ya buluu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Abay)
Mto wa Nile ya buluu (Ethiopia: Abbai)
Maporomoko ya Tis Issat ya Nile ya buluu
Chanzo Ziwa Tana (chemchemi ya Gishe Abbai)
Mdomo Mto Nile mjini Khartum (Sudan)
Nchi Ethiopia, Sudan
Urefu 1.350 km
Kimo cha chanzo 1830 m
Mkondo ?? m³/s
Eneo la beseni 326,400 km²
Ramani ya Nile ya buluu

Nile ya buluu ni tawimto kubwa la mto Nile. Inaanza katika Ziwa Tana kwenye nyanda za juu za Ethiopia na kutelemka hadi Sudan. Mdomo wake uko mjini Khartum inapounganika na Nile nyeupe na kuunda mto wa Nile wenyewe.

Kwa jumla Nile ya bluu inabeba maji mengi kushinda Nile nyeupe.

Ndani ya Ethiopia mto huitwa kwa jina Abbai (mto mkubwa, pia Abay au Abai) kwa kuwa ndio mto mkubwa kabisa wa Ethiopia.

Baada ya kutoka Ethiopia na kuingia Sudan inaitwa kwa Kiarabu: النيل الأزرق; an-nīl al-azraq.

Ina chanzo chake kwenye kimo cha mita 1800 juu ya UB inapotoka katika Ziwa Tana katika nyanda za juu za Ethiopia. Kwanza inaelekea kusini-mashariki lakini inabadili mwelekeo kwenda magharibi halafu kaskazini.

Waethiopia wengi wanasemekana kuutazama kama mto mtakatifu.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nile ya buluu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.