Tana (ziwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ziwa Tana)
Ziwa la Tana
Ziwa la Tana, picha kutoka angani, 1991
Ziwa la Tana, picha kutoka angani, 1991
Mahali Nyanda za juu za Ethiopia, (Afrika ya Mashariki)
Eneo la maji 2.156 km²
Kina cha chini 14 m
Mito inayoingia Rib na Gumara
Mito inayotoka Abbai (Nile ya buluu)
Kimo cha uso wa maji
juu ya UB
1.788 m
Miji mikubwa ufukoni Bahir Dar

Ziwa la Tana ni ziwa kubwa la Ethiopia na asili ya Nile ya Buluu. Beseni yake iko taktiban 370 km kaskazini-magharbibi ya Addis Ababa katika nyanda za juu za Ethiopia.

Umbo la ziwa limebadilika katika karne iliyopita kutokana na mashapo. Kamusi ya mwaka 1888 ilitaja kina ya mita 100, lakini leo ni mita 14 pekee. Eneo la ziwa hubadilika na majira ya mvua au ukame yaani kuwa na maji mengi au kidogo. Mito mingi inaingia ziwani ikiwa mikubwa kati yao ni mito ya Rib na Gumara.

Mto wa Abbai (jina la Kiethiopia la Nile ya buluu) unatoka katika ziwa.

Eneo la Ziwa la Tana ni kitovu cha kihistoria cha Ethiopia ya Kikristo. Katika visiwa vidogo ziwani kuna makanisa na monasteri 20 zilizojengwa tangu karne ya 14 BK.

Picha[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tana (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.