Msikiti wa Umawiya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Uwanja wa msikiti wa Umawiya
Kaburi la kichwa cha Yohane Mbatizaji ndani ya msikiti

Msikiti wa Umawiya (Kiarabu: جامع بني أمية jami'a bani umaya) ni msikiti mkuu mjini Dameski katika Syria. Ni moja kati ya misikiti ya kale kabisa ilijengwa kati ya 695 hadi 705 BK. Kabla ya ujenzi wa msikiti mahali palikuwa na kanisa la Mt. Yohane Mbatizaji lililobomolewa kwa amri ya Al-Walid aliyekuwa khalifa wa sita katika nasaba ya Waumawiya.

Mabaki ya kanisa na hekalu ndani ya msikiti[hariri | hariri chanzo]

Ndani ya msikiti kuna kaburi la kichwa cha Yohane mbatizaji kilichotunzwa hata baada ya kubomolewa kwa kanisa. Kanisa hli liliwahi kujengwa juu ya hekalu kubwa ya Jupiter na hadi leo sehemu ya kuta za nje ni zilezile za hekalu ile ya kale.

Picha za msikiti[hariri | hariri chanzo]

Uwanja ndani ya msikiti imepambwa kwa picha za mosaiki zinazoonyesha miti, majani na majengo kufuatana na mtindo wa Kibizanti na wasanii walikuwa wataalamu Wakristo walioajiriwa kwa kazi hii. Lakini hakuna picha za watu au wanyama kulingana na kanuni za Kiislamu ingawa hata picha jinsi zilivyo hapa hazikuwekwa katika misikiti za baadaye.

Kando la msikiti kuna kaburi la Sultani Salah ad-Din.