Nenda kwa yaliyomo

Salah ad-Din

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Salah ad-Din, picha katika kitabu cha Kiarabu cha karne ya 12

Salah ad-Din al-Ayubi (11384 Machi 1193; pia: Saladin) alikuwa mtawala wa Misri na Syria wakati wa karne ya 12. Anakumbukwa hasa kwa ushindi wake juu ya Wamisalaba na ufalme wao wa Yerusalemu. Aliunda nasaba ya Waayubi walioendelea kutawala Misri pamoja na Yemeni, Shamu, Iraq na Hijaz.

Kupanda ngazi kama mwanajeshi[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa katika familia ya Wakurdi babake alikuwa mwanajeshi katika utumishi wa Sultani wa Dameski. Alipokuwa na umri wa miaka 25 alitumwa Misri kwa vita dhidi ya Khalifa wa Wafatima. Misri alipanda ngazi akawa waziri au mkuu wa serikali ya Misri.

Sultani wa Misri[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kifo cha khalifa wa mwisho Salah ad-Din alitwaa mamlaka akajipa cheo cha Sultani na kutawala Misri.

Kutwaa Shamu na Yerusalemu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1174 alivamia Shamu na kuunga Syria na milki yake. Akaipanusha hadi Aleppo (1183) na Mosul (1186) akaendelea kushambulia ufalme wa Yerusalemu wa Wamisalaba.

4 Julai 1187 alishinda jeshi la Wamisalaba na kutwaa mji wa Yerusalemu akimaliza utawala wa Wakristo uliowahi kudumu miaka 88.

Mapigano ya Hattin 1191 wakati wa Vita ya tatu ya misalaba

Vita ya tatu ya Wamisalaba[hariri | hariri chanzo]

Mataifa wa Ulaya yalikusanya jeshi jipya dhidi yake na kwenda kwa vita ya tatu ya misalaba. 1191 Mfalme Richard I wa Uingereza alimshinda Salah ad-Din na pande zote mbili walipatana kupumzisha silaha. Walipatana ya kwamba Yerusalemu itabaki mkononi mwa Waislamu lakini Wakristo watakuwa huru kuhiji huko na kutembelea mji pamoja na mahali pa kumbukumbu ya Yesu. Ufalme wa Wamisalaba uliendelea kushika kanda la pwani la Palestina.

Kifo mjini Dameski[hariri | hariri chanzo]

Tar. 3 Machi 1193 Salah ad-Din aliaga Dunia mjini Dameski akiwa na umri wa miaka 55. Kaburi lake limetunzwa hadi leo liko kando la msikiti wa Umawiya.