Mgongo kati wa Atlantiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mid-Atlantic Ridge)
Ramani ya mgongo kati ya Atlantiki.

Mgongo kati wa Atlantiki (kwa Kiingereza: Mid-Atlantic Ridge) ni safu ya milima chini ya maji ya bahari ya Atlantiki inayoelekea kutoka 87°N (km 333 kusini kwa Ncha ya kaskazini) hadi kisiwa cha Bouvet kusini mwa dunia kwenye 54°S.

Vilele vya juu vya milima hiyo vinaonekana juu ya UB kama visiwa. Safu hiyo ya milima imetokea mahali ambako mabamba ya gandunia yanaachana: bamba la Ulaya-Asia na bamba la Amerika ya Kaskazini katika Atlantiki ya Kaskazini, halafu bamba la Amerika ya Kusini na bamba la Afrika katika Atlantiki ya Kusini.

Mabamba hayo yana mwendo wa kuachana na katika nafasi kati yake magma hupanda juu inayokuwa mwamba mpya uliosababisha kutokea kwa milima ya safu.

Kutambuliwa kwa safu hiyo kuliweka msingi kwa nadharia ya upanuzi wa misingi ya bahari unaosababisha mwendo wa mabamba ya gandunia.

Magma inapanda juu penye kuachana kwa mabamba ya gandunia na kujenga safu za milima ya migongo chini ya bahari.

Visiwa vya mgongo kati wa Atlantiki[hariri | hariri chanzo]

Visiwa ambavyo ni vilele vya milima ya mgongo huo ni kama vifuatavyo (katika mabano ni majina ya vilele vya juu na kimo):

Nusudunia ya kaskazini (Atlantiki ya Kaskazini)[hariri | hariri chanzo]

  1. Jan Mayen (Beerenberg, m 2277)
  2. Iceland (Hvannadalshnúkur in the Vatnajökull, m 2,109.6)
  3. Azori (Ponta do Pico au Pico Alto kwenye kisiwa cha Pico, m 2,351)
  4. Bermuda (Town Hill kwenye kisiwa cha Main Island, m 76)
    (Bermuda ilianza juu ya mgongo lakini imesogea mbali sasa)
  5. Saint Peter and Paul Rocks (Southwest Rock, m 22.5)

Nusudunia ya kusini (Atlantiki ya Kusini)[hariri | hariri chanzo]

  1. Kisiwa cha Ascension (The Peak, Green Mountain, m 859)
  2. Tristan da Cunha (Queen Mary's Peak, m 2062)
  3. Kisiwa cha Gough (Edinburgh Peak, m 909)
  4. Kisiwa cha Bouvet (Olavtoppen, m 780)
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.