Mesrop

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mesrop Mashtots alivyochorwa mwaka 1776.
Mesrop Mashtots alivyochorwa na Francesco Maggiotto (1750-1805).
Monasteri ya Amaras huko Nagorno Karabakh ambapo Mesrop Mashtots alianzisha shule ya kwanza iliyotumia alfabeti yake.[1]

Mesrop Mashtots (pia Mesrob Mashtotz, kwa Kiarmenia Մեսրոպ Մաշտոց; Hatsik 361 - Echmiadzin 17 Februari 440) alikuwa mmonaki, mwanateolojia na mtaalamu wa lugha kutoka Armenia aliyebuni alfabeti ya Kiarmenia (406) na kuanzisha shule nyingi akiweka hivyo misingi ya taifa hilo na ustaarabu wake uliolidumisha hata leo kati ya matatizo makubwa ya historia yake, hasa dhuluma za kidini.

Ni kwamba Mesrop alianzisha mtindo wa monasteri kuwa na shule karibu nayo ili kuandaa watu watakaoendeleza elimu ya dini hasa kwa kutafsiri na kunakili vitabu.

Mapema monasteri kubwa zikawa pia na seminari kuu au vyuo vikuu vya teolojia.

Hivyo umonaki wa Armenia ulidumisha utamaduni wa taifa hilo, ambalo lilikuwa la kwanza kupokea Ukristo jumla pamoja na mfalme wake (300) halafu likaushika moja kwa moja hata lilipopitia vipindi vigumu sana.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Viviano, Frank. “The Rebirth of Armenia,” National Geographic Magazine, March 2004
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.