Seminari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Seminari kuu)
Rukia: urambazaji, tafuta

Seminari ni muundo wa malezi unaotoa mafunzo ya dini, hususan Ukristo, yakiwa pengine pamoja na elimu dunia.

Seminari kuu, au vyuo vya teolojia, ni muundo wa malezi ya juu kwa watu wanaolenga upadri au huduma nyingine ya uongozi katika Kanisa.

Tofauti na hiyo, seminari ndogo inalea vijana kuanzia baadhi ya madarasa ya shule ya msingi hadi vidato vya sekondari.

Neno linatokana na Kilatini: seminarium ina maana ya kitalu, mfano uliotumiwa na Mtaguso wa Trento katika hati Cum adolescentium aetas ambayo ilianzisha seminara za kwanza za kisasa.[1]

Baada ya muundo huo kuenea katika Kanisa Katoliki, hata madhehebu mengine na hatimaye dini nyingine vimeanza kutumia mbinu hiyo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. XXIII Session, Council of Trent, ch. XVIII. Retrieved from (1848) in J. Waterworth: The Canons and Decrees of the Sacred and Oecumenical Council of Trent. London: Dolman, 170–92. Retrieved on June 16, 2009.