Melesyo wa Antiokia
Melesyo wa Antiokia (Melitene, Armenia ya Kale, karne ya 3 au ya 4 - Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 381) alikuwa askofu wa Sebaste, halafu akawa askofu mkuu wa mji huo kuanzia mwaka 360 hadi kifo chake ingawa alifukuzwa mara tatu kwa kupinga Uario[1].
Alifariki akiwa anasimamia mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli.
Gregori wa Nisa na Yohane Krisostomo walimsifu sana kwa maadili yake.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 12 Februari[2].
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |