Maria Zhou Wuzhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wafiadini Wakatoliki wa China.

Maria Zhou Wuzhi (Zhujiahe, 1850 hivi - Zhujiahe, 20 Julai 1900) alikuwa mwanamke wa China aliyefia Ukristo wakati wa Uasi wa Waboksa. Alipoona wamevamia kanisa, na kutaka kumchoma padri Leo Ignas Mangin aliyekuwa anaongoza ibada, alijaribu kumkinga kwa mwili wake akajeruhiwa akafa. Pamoja nao aliuawa Paulo Denn [1].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.

Sikukuu yao ya pamoja huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake [2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.