Nenda kwa yaliyomo

Leo Ignas Mangin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha yake halisi.

Leo Ignas Mangin, S.J. (Verny, Ufaransa, 30 Julai 1857 - Zhujihae 20 Julai 1900) alikuwa padri wa Ufaransa mmisionari nchini China aliyefia Ukristo huko wakati wa Uasi wa Waboksa waliovamia kanisa alimokuwa anawatia moyo waamini wakamchoma mbele ya altare pamoja na Paulo Denn na Maria Zhou Wuzhi [1].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 mwaka 2000.

Sikukuu yao ya pamoja huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 20 Julai[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.