Margaret Ward
Margaret Ward (Congleton, 1550; Tyburn, 30 Agosti 1588) alikuwa mwanamke wa Uingereza aliyeuawa kwa sababu ya imani yake katika dhuluma za serikali ya nchi hiyo dhidi ya Kanisa Katoliki.
Dhuluma hiyo ilianzishwa na Malkia Elizabeti I (1533-1603) na kuendelezwa na waandamizi wake kwa ukali wa kiwango tofauti, hasa miaka 1535-1679.
Pamoja na kutambua hatari ya kuwa Mkatoliki, Margaret alimsaidia padri William Watson, aliyewahi kufungwa na kuteswa mara kadhaa ili aasi Kanisa lake na kujiunga na Anglikana.
Ingawa Margaret alimtembelea mara nyingi, hatimaye padri huyo aliasi ili kurudishiwa uhuru wake. Lakini baadaye alijuta sana akaamua kukana hadharani uamuzi wake huo, hivyo akafungwa tena huko Bridewell.
Hapo Margaret alimsaidia kutoroka gerezani, lakini aligharimu mwenyewe ujasiri huo. Alipelekwa mahakamani ambapo hakukanusha tendo lake, hakukana imani yake wala hakuomba msamaha wa malkia. Hivyo alihukumiwa kuuawa kwa usaliti pamoja na Wakatoliki wengine, wakiwemo mapadri na walei, akapokea kwa furaha adhabu ya kunyongwa[1].
Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Desemba 1929, na Papa Paulo VI alimtangaza mtakatifu tarehe 25 Oktoba 1970.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |