Nenda kwa yaliyomo

Mapigano ya Marathoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uchoraji wa kisasa unaolenga kuonyesha mapigano ya Marathoni

Mapigano ya Marathoni (kwa Kiingereza: Battle of Marathon) yalifanyika mnamo Septemba 490 KK kwenye uwanda wa Marathoni, si mbali na Athens, Ugiriki. Yalipigwa kati ya jeshi la Athens na Waajemi. Athens iliungwa mkono na kikosi kidogo kutoka mji wa Plataia. Ushindi wa Athens ulimaliza jaribio la kwanza la Uajemi ya Kale kupata kipaumbele katika Ugiriki.

Uvamizi wa Uajemi ulikuwa jibu la ushiriki wa Athens katika uasi wa Ionia. Hapo miji ya Athens na Eretria iliwahi kutuma kikosi kusaidia miji ya Ionia, ambayo ilikuwa ikijaribu kupindua utawala wa Uajemi. Waathens na Eretria walifanikiwa kukamata na kuchoma Sardis (makao makuu ya gavana wa Uajemi)[1], lakini walilazimika kurudi nyuma na hasara kubwa. Kwa kujibu uvamizi huu, mfalme Dario I wa Uajemi aliapa kuchoma Athens na Eretria.

Uvamizi wa Waajemi

[hariri | hariri chanzo]

Mara tu uasi wa Ionia ulipoangamizwa na Waajemi, mfalme Dario alianza kupanga adhabu ya miji ya Kigiriki waliompinga. Mnamo 490 KK alituma kikosi chini ya majenerali Datis na Artaphernes waliovuka Bahari ya Aegean, ili kuteka Visiwa vya Kikladi katika bahari hiyo. Hatua iliyofuata ilikuwa kushambulia mji wa Eretria. Waajemi wakakamata na kuchoma Eretria.

Kutoka hapo Waajemi walipanda meli zao kwenda Attika, rasi kubwa ya Ugiriki ambako Athens iko. Walifika kwenye hori ya Marathoni.

Mapigano

[hariri | hariri chanzo]
Mahali pa Marathoni (A= Athens)

Marathoni pana uwanja mpana uliofaa kwa jeshi lao maana ilikuwa na tambarare ambako jeshi la farasi lilipewa nafasi nzuri. Waathens, waliojiunga na kikosi kidogo kutoka mji wa Plataia, walikimbia kwenda Marathoni walipofaulu kuzuia njia kutoka katika tambarare ya Marathoni. Majeshi yalitazamana kwa siku tano hivi.

Hali halisi si rahisi kuelewa kutokana na taarifa zilizohifadhiwa ambazo zote ziliandikwa kitambo baadaye. Hatimaye Wagiriki walishambulia Waajemi. Inawezekana shambulio hilo lilitokea wakati farasi wa Waajemi walihamishwa tena kwenye meli kwa sababu jemadari Mwajemi aliamua kuhama. Kwa namna yoyote, jeshi la farasi upande wa Waajemi halikushiriki katika mapigano na askari wa Athens wenye nguo za kinga walishinda wanajeshi wa miguu wa Waajemi waliokuwa na silaha nyepesi zaidi.   Walipiga mabawa ya Uajemi kabla ya kugeukia katikati ya mstari wa Uaji. Waathens walikamata manowari saba lakini manowari nyingine ziliweza kukimbia. Athens ilipoteza raia 192 lakini haijulikani walipoteza watumwa na watu wengine wasiokuwa raia huru. Waajemi walisemekana kupoteza watu 6000.

Ushindi wa Marathoni ulikuwa mwisho wa jaribio la kwanza la Uajemi kuvamia Ugiriki. Jeshi la Kiajemi lilirudi upande wa Asia Ndogo. Mfalme Dareio alikuwa na hasira akaanza kuandaa jeshi kubwa kwa kulipiza kisasi, lakini mnamo mwaka 486 KK uasi huko Misri -sehemu ya Dola la Uajemi- ulimlazimisha kuachana na mipango hiyo. Baada ya kifo cha Dario, mwana na mwandamizi wake Xerxes I aliandaa uvamizi mwingine wa Ugiriki ulioanza mnamo 480 KK.

Asili ya Mbio za Marathon

[hariri | hariri chanzo]
Helmeti ya Kigiriki pamoja na sehemu ya fuvu zilizopatikana kwa njia ya uchimbaji wa kiakiolojia kwenye uwanda wa Marathoni

Kufuatana na hadithi inayosimuliwa mahali pengi, kijana alikimbia kutoka Marathoni hadi Athens kuleta habari za ushindi. Hadithi hiyo ni chanzo cha Mbio ya Marathoni ambao ni mbio ya urefu mkubwa wa km 42.195 katika riadha ya kimataifa na sehemu ya mashindano wakati wa Michezo ya Olimpiki ya kisasa.

Masimulizi hayo si ya kihistoria; msingi wake ni taarifa ya Herodoti aliyeandika kwamba kijana alitumwa kutoka Athens kwenda Sparta kuomba msaada dhidi ya uvamizi wa Uajemi; kijana huyu alipita kilomita 225 hadi Sparta akafika siku iliyofuata. Halafu katika kisa tofauti, Herodoti aliandika kwamba jeshi la Athens baada ya mapigano lilirudi kwa kasi kubwa iwezekanavyo kilomita 40 kutoka Marathon hadi Athens kwa sababu walihofia Waajemi wangejaribu kuvamia mji kwa njia ya meli zao[2]; walipofika jioni waliona jahazi za Waajemi zikikaribia. Lakini Waajemi walipotambua jeshi la Athens lilikuwa limerudi na kuwa tayari, walirudi kwao.[3]

Baadaye, lakini tayari nyakati za Roma ya Kale, masimulizi hayo yaliunganishwa kuwa moja ambako kijana (aliyepewa mara nyingi jina la Philippides) alikimbilia Athens kupeleka habari za ushindi; katika simulizi hilo aliweza kutamka "Tumeshinda" kabla ya kuanguka chini na kufa kwa uchovu. Wakati michezo ya Olimpiki ilipoanzishwa upya katika karne ya 19, hadithi hiyo ilifufuliwa na kuwa msingi kwa mashindano ambako wakimbiaji wanashindana kwa urefu wa kilomita 41.195 kwenye mbio za Marathon.[4]

  1. Herodoti, Kitabu cha 5: Terpsichore [100
  2. Herodoti 6, 115
  3. Herodoti 6, 116
  4. [aimsworldrunning.org/marathon_history.htm Marathon History], tovuti ya Association of International Marathons and Distance Races, iliangaliwa 2020
  • Herodotus, the Histories, with an English translation by A. D. Godley. Cambridge. Harvard University Press. 1920 (online hapa)

Utaalamu wa kisasa

[hariri | hariri chanzo]
  • Hans W. Giessen, Mythos Marathon. Von Herodot über Bréal bis zur Gegenwart. Verlag Empirische Pädagogik, Landau (= Landauer Schriften zur Kommunikations- und Kulturwissenschaft. Band 17) 2010. ISNB 978-3-941320-46-8
  • Green, Peter (1996). The Greco-Persian Wars. University of California Press. ISBN 0-520-20313-5.
  • Holland, Tom (2006). Persian Fire: The First World Empire and the Battle for the West. Abacus. ISBN 0-385-51311-9.
  • Lacey, Jim. The First Clash: The Miraculous Greek Victory at Marathon and Its Impact on Western Civilization (2011), popular
  • Lagos, Constantinos. Karyanos Fotis, Who Really Won the Battle of Marathon? A Bold Re-Appraisal of One of History's Most Famous Battles, Pen and Sword, Barnsley, 2020, (ISNB 978-1526758064)
  • Lazenby, J.F. The Defence of Greece 490–479 BC. Aris & Phillips Ltd., 1993 (ISNB 0-85668-591-7)
  • Lloyd, Alan. Marathon: The Crucial Battle That Created Western Democracy. Souvenir Press, 2004. (ISNB 0-285-63688-X)
  • Davis, Paul. 100 Decisive Battles. Oxford University Press, 1999. ISNB 1-57607-075-1}}
  • Powell J., Blakeley D.W., Powell, T. Biographical Dictionary of Literary Influences: The Nineteenth Century, 1800–1914. Greenwood Publishing Group, 2001. ISNB 978-0-313-30422-4}}
  • Fuller, J.F.C. A Military History of the Western World. Funk & Wagnalls, 1954.
  • Fehling, D. Herodotus and His "Sources": Citation, Invention, and Narrative Art. Translated by J.G. Howie. Leeds: Francis Cairns, 1989.
  • Finley, Moses (1972). "Introduction". Thucydides: History of the Peloponnesian War. Ilitafsiriwa na Rex Warner. Penguin. ISBN 0-14-044039-9.
  • D.W. Olson et al., Sky & Telescope Sep. 2004
  • Krentz, Peter. The Battle of Marathon. Yale University Press, 2010
  • Lanning, Michael L. (Aprili 2005). "28". The Battle 100: The Stories Behind History's Most Influential Battles. Sourcebooks. ku. 95–97. ISBN 978-1402202636.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Davis, Paul K. (Juni 2001). "Marathon". 100 Decisive Battles: From Ancient Times to the Present. Oxford University Press. ISBN 978-0195143669.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Roisman, Joseph; Worthington, Ian (2011). A Companion to Ancient Macedonia. John Wiley and Sons. ISBN 978-1-44-435163-7.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mapigano ya Marathoni kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.