Madonda matakatifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mikono ya Yesu na Fransisko yenye Stigmata ni nembo ya Ndugu Wadogo; Linz, Austria.
Katerina wa Siena akizimia kutokana na madonda matakatifu: mchoro wa Il Sodoma, Alsace, Ufaransa.

Madonda matakatifu (kwa Kilatini na Kiingereza Stigmata, wingi wa stigma, kutoka Kigiriki στίγμα) ni jina linalotumiwa na Wakristo kutaja majeraha au maumivu katika viungo vya mwili ambapo Yesu alipatwa na madonda 5 wakati wa kusulubiwa, yaani mikono, miguu na ubavu, lakini pia kichwa na sehemu nyingine alipotiwa taji la miiba au kupigwa mijeledi.

Mtume Paulo mwishoni mwa Barua kwa Wagalatia aliandika, "Mimi nachukua mwilini mwangu chapa (stigmata) za Yesu."[1] kama zile zinazotiwa juu ya mwili wa wanyama au watumwa ili kutambua ni mali ya nani. Inafikiriwa kwamba alikuwa anadokeza alama za mapigo aliyoyapata kwa ajili ya imani yake.

Watu waliopata alama za namna hiyo lakini bila mapigo ya kawaida walitokea hasa katika watawa wa Kanisa Katoliki kama vile Wadominiko na Wafransisko.[2]

Wa kwanza kujulikana ni shemasi Fransisko wa Asizi. Padri wa kwanza ni Pio wa Pietrelcina.

Asilimia 80 ni wanawake.[3]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Jones, C.P. (1987) Stigma: Tattooing & Branding in Graeco-Roman Antiquity. J. Roman Studies 77, 139-155.
  2. Poulain, A. (1912). Mystical Stigmata. In The Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. Retrieved July 1, 2008 from New Advent: http://www.newadvent.org/cathen/14294b.htm
  3. Catholic cults and devotions: a psychological inquiry by Michael P. Carroll 1989 ISBN 0-7735-0693-4 pages 80-84

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Christianity Symbol.png Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Madonda matakatifu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.